Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

by Admin | 6 December 2021 08:46 pm12

Tuwasome,

Walawi 11:13 “Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;

14 na mwewe, na kozi kwa aina zake,

15 na kila kunguru kwa aina zake;

16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa;

18 na mumbi, na mwari, na mderi;

19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo”.

  1. TAI

Tai ni ndege maarufu anayejulikana kwa uwezo wake wa kuona mbali, na vile vile mwenye uwezo wa kuruka juu zaidi ya ndege wengine wote, Mvua inaponyesha na mawingu kutanda, Tai hupaa juu ya mawingu, na baadaye kushuka chini mvua inapoisha, tofauti na ndege wengine wote ambao mawingu yanapotanda tu!, wanakimbilia viota vyao kujisitiri.(Tazama picha chini).

Tai

  1. FURUKOMBE

Furukombe au kwa kiingereza “Vulture”  ni aina nyingine ya ndege ambao kimwonekano wanakaribia kufanana na Tai, isipokuwa hawa wana midomo mirefu kidogo, na pia wanakula Mizoga ya wanyama waliokufa maporini (Tazama picha chini), rangi yao ni rangi ya kahawia.

Furukombe

  1. KIPUNGU

Kipungu ni aina iyo hiyo ya Furukombe, isipokuwa kipungu ni mweusi, tabia zake ni kama za Furukombe wa kahawia, anakula mizoga, tofauti na Furukombe, kipungu yeye anapatikana nchi za ukanda wa baridi.(Tazama picha chini)

kipungu

  1. MWEWE

Mwewe ni jamii ya Tai, na ni ndege maarufu wenye rangi ya kahawia na wanapatikana na kuonekana sana maziringira wanayoishi wanadamu. Mwewe naye huruka juu sana, lakini si kama Tai, anapatikana sana sehemu za joto, na chakula chake kikuu ni ndege wengine wadogo wadogo, kama mashomoro pamoja na vifaranga vya kuku. (Tazama picha chini).

mwewe

  1. KOZI

Kozi ni Mwewe mweusi, Huyu hana tofauti na Mwewe wa kahawia kitabia, kilichowatofautisha ni rangi tu!, na ukubwa. Kozi yeye kiumbile ni mdogo kuliko Mwewe, na mkia wake ni mfupi. (Tazama picha chini).

KOZI

  1. KIRUKANJIA

Kirukanjia ni aina ya “Bundi” wenye manyoya kama mapembe kwenye vichwa vyao, (Tazama picha chini).

kirukanjia

  1. DUDUMIZI

Dudumizi ni aina ya ndege weupe wanaoishi kwenye fukwe za bahari, ambao wana miguu iliyofungamana kama bata, chakula chao kikubwa ni samaki. (Tazama picha chini).

Dudumizi

  1. KIPANGA

Kipanga ni ndege anayekaribia kufanana sana na Mwewe, isipikuwa yeye kimwonekano ni mdogo, tabia za kipanga ni kama za mwewe, chakula chake ni kama cha mwewe,(yaani kula ndege wengine wadogo ikiwemo vifaranga vya kuku).

kipanga

  1. MNANDI

Mnandi ni aina ya ndege wanakaribia kufanana na Dudumizi, isipokuwa Mnandi wanaishi kando kando ya maziwa na mito, na chakula chao kikubwa ni samaki kama walivyo dudumizi, na kimwonekano ni wausi.

mnandi

  1. MUMBI

Mumbi ni bundi mweupe, (Tazama picha chini).

mumbi

  1. MWARI

Mwari ni bundi wa jangwani. (Tazama picha chini).

Mwari

  1. MDERI      

Mderi ni jamii ya Mwewe wanaokula samaki. . (Tazama picha chini)

mderi

  1. KORONGO

Korongo ni jamii ya ndege weupe wenye midomo mirefu na miguu mirefu iliyo membamba, wanaishi kando kando ya mito na mabwawa, chakula chao kikubwa ni samaki na nyoka. (Tazama picha chini).

korongo

  1. KOIKOI

Koikoi ni jamii ya ndege wadogo, wenye sifa ya kusafiri umbali mrefu >Kwa maelezo marefu juu ya ndege hawa koikoi na somo gani wamebeba kiroho fungua hapa>> Koi koi.

  1. HUDI HUDI

Hudi hudi ni aina ya ndege, wenye kichwa kilichochongoka na wenye rangi mbali mbali kwenye manyoa yao..

hudi hudi

Hiyo ndiyo orodha ya ndege ambayo Bwana Mungu aliwakata wana wa Israeli wasiwale. Kulikuwepo na wanyama wengine kama Nguruwe, Sungura, ngamia na wengine baadhi, ambao pia wana wa Israeli hawakuruhusiwa kuwala..

 Bwana Mungu alitumia tabia za wanyama hao kutaka kufundisha jambo fulani la kiroho, ambalo sisi watu wa agano jipya tumeweza kulielewa, hivyo kwasasa hakuna tena kilicho najisi, vyote vimetakaswa.

Sasa kuelewa ni somo gani lilikuwa nyuma ya viumbe hao, mpaka kufikia Bwana Mungu kuwakataza Israeli wasiwale, unaweza kufungua hapa >>> Je tunaruhisiwa kula nyama ya Nguruwe?

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Lumbwi ni nini katika biblia?

Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

MAMA, TAZAMA, MWANAO.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/12/06/hawa-ndege-waliotajwa-katika-walawi-1113-19-kuwa-ni-najisi-ndio-ndege-gani-kwasasa/