Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?

by Admin | 19 January 2022 08:46 am01

Mjoli ni mfanyakazi-mwenza, Ni mtu unayefanya naye kazi moja inayofanana.. Kwamfano kama wewe ni mwalimu, ukakutana na mwalimu mwenzako huyo ni mjoli wako…Kama wewe ni mhubiri ukakutana na mhubiri mwenzako huyo ni mjoli wako, kama wewe ni mkulima ukakutana na mkulima mwenzako huyo ni mjoli wako..

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia..

Mathayo 18:23-35
[23]Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
[24]Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta
elfu kumi.
[25]Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.
[26]Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
[27]Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
[28]Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari
mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.
[29]Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
[30]Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.
[31]Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
[32]Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
[33]nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?
[34]Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.
[35]Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Wafilipi 4:3
[3]Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.

Soma pia..Wakolosai 1:7 ,4:7, Ufunuo 19:10, 22:9.

Vivyo hivyo na sisi watakatifu ulimwenguni kote tuliookolewa na Yesu Kristo, kila mmoja ni mjoli kwa mwenzake. Hivyo hatuna budi kupendana, kutumikiana, kusameheana.. Maadamu tupo katika shamba moja na kazi moja, tunapaswa kuujenga ufalme wa Mungu kwa nguvu zetu zote. Huku tukizingatia misingi ya Biblia, na sio ya kidhehebu au kidini

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?

Makuruhi ni nini, kama tunavyosoma katika biblia?

JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/01/19/mjoli-ni-nini-ni-nani-katika-biblia/