by Admin | 24 January 2022 08:46 am01
SWALI: BWANA YESU asifiwe mtumishi, mistari hii inanichanganya nisielewe vizuri, Neno la Mungu linasema;
Hesabu 23:19
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Hapa biblia inasema hasemi uongo Wala hajuti, lakini ukisoma tena hapa inasema
1 Samweli 15:11
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.
Nashindwa kuutambua ukweli Ni upi?
JIBU: Ukweli ni kwamba Mungu HAJUTI..Isipokuwa kuna wakati anajiweka katika mazingira ya kibinadamu ili tuzielewe hisia zake vema.
Na ndio maana mahali pengine utaona anazionyesha kazi zake kama vile zinamapungufu fulani, hazijakamilika..mpaka anatumia neno SI VEMA huyu mtu aishi peke yake nitamfanyia msaidizi, kana kwamba hakuliona hilo tangu mwanzo, lakini ukisoma mwanzoni kabisa katika kitabu cha Mwanzo 1:27 inatuambia tayati alishamuumba mwanaume na mwanamke katika mawazo yake..lakini katika utekelezaji anajifanya kama kasahau, ndio hapo anakuja kumuumba mwanamke baadaye sana baada ya uumbaji wote kukamilika Mwanzo 2:8..
Hiyo ndio tabia ya Mungu. Anajiweka hivyo wakati mwingine ili kutufundisha sisi jambo.
Mara nyingine anajifanya kama hana mashauri bora ya kumzidi mwanadamu..utakumbuka kule jangwani Musa alimshauri Mungu aghahiri mawazo yake..lakini haimaanishi kuwa Mashauri yetu ni zaidi ya Mungu. Soma Kutoka 32:9-14
Halikadhalika hapa..anasema..yeye si mwanadamu hata ajute..ikiwa na maana mipango yake yote tayari alishaiona mwisho wake utakuwaje tangu mwanzo..kwamba huu utaishia katika uzuri au huu utaishia pabaya..kwamfano alipomuumba shetani, alijua kabisa ataasi, na atawapoteza malaika na wanadamu wengi..lakini akamuumba hivyo hivyo..
Hata sasa Mungu anajua kabisa mwisho wa kila mwanadamu na kila jambo..kwamfano katika habari hiyo ya Sauli..Mungu alijua atakuja kukengeuka huko mbeleni..lakini alimpa bado ufalme..
Na alipokuja kukengeuka kweli, ndio tunaona Mungu anamwambia Samweli najuta kwanini nimechagua Sauli awe mfalme..kuonyesha tu hisia zake juu ya Sauli ili sisi wanadamu tumuelewe. Lakini alifahamu kila kitu.
Halikadhalika hata sasa mambo kama hayo Mungu anayafanya rohoni, .Mungu kukusifia leo haimaanishi kuwa ndio tiketi ya mbinguni moja kwa moja…Mungu kukutia mafuta sasa na kuwaacha wengine, haimaanishi kuwa wewe ndio kipendwa cha Bwana, hata ukifanya dhambi atakusitiri tu siku ile kisa ni kuhani wake.
Ukweli ni kwamba wapo watu ambao wataishia kuwa manabii wa uongo, wengine wapinga-kristo, na jehanamu wataenda..lakini ushuhuda wa wito watakuambia ni Yesu mwenyewe alinitokea na kunituma..Akanipa na ishara za miujiza, lakini wanaishia motoni
Mathayo 7:21-23
[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Swali ni je…umempa Kristo maisha yako na kusimama kweli kweli? Unahabari kuwa Karama pekee sio uthibitisho kuwa Mungu yupo na wewe? Wakati wowote anaweza kujutia na kughahiri huo wito wako, aliokupa kama unasua sua
Kama hujasimama imara, fanya hivyo sasa. Mgeukie muumba wako kwa kumaanisha kwasababu, kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo mlangoni kurudi
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/01/24/je-mungu-huwa-anajuta/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.