Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).

by Admin | 30 January 2022 08:46 pm01

Kibiblia mzushi ni mtu anayezusha jambo au mada ambazo lengo lake ni kuleta MIGAWANYIKO!.

Mtu anayezuka katikati ya kanisa na kuzusha mada ambazo anajua kabisa zitaishia kuleta migawanyiko ndani ya kanisa la Kristo, mtu huyo ni Mzushi kibiblia. Kwa lugha ya kiingereza (divisive person).

Na biblia imetoa maelekezo juu ya watu hao, kwamba tuwakatae, (maana yake tusiwape nafasi).

Tito 3:10 “Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;

11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe”.

Mfano wa mada zinazoleta migawanyiko ndani ya kanisa ndio hizo Mtume Paulo alizoziorodhesha katika Tito 3:9..

Tito 3:9 “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana”.

Mashindano ya dini, hayo yanasababisha kiburi na mwishowe migawanyiko katika kanisa kwasababu yanawaharibu wale wanaosikia…

Kwasababu ndani ya kanisa kuna ambao pia bado ni wachanga katika Imani, sasa endapo wakisikia watu wanashindana (kila mmoja anajiona mjuzi) ni rahisi Imani zao kudhoofika na hata kuiacha ile Imani, au kuegemea upande mmoja na kuudharau mwingine, hivyo tayari migawanyiko imeshaingia.

2Timotheo 2:14 “Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao”.

1Timotheo 6:4 “..amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya”

Na sisi kama wakristo hatuna budi kujihadhari na Uzushi, vile vile watu ambao ni wazushi katika kanisa, baada ya kuwaonya mara ya kwanza na ya pili, na hawataki kubadilika maandiko yametupa ruhusu ya kujiepusha nao!, maana yake kutowapa nafasi yoyote ya kusema au kuchangia chochote!, wabaki kimya au wazungumze wao wenyewe.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

UFUNUO Mlango wa 2: Sehemu ya pili.

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.

Neno “Uchungu wa mauti” lina maana gani kibiblia?

TWAENENDA KWA IMANI NA SI KWA KUONA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/01/30/mzushi-ni-nani-kibiblia-tito-310/