Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?

by Admin | 19 February 2022 08:46 pm02

Kigao ni aina ya silaha inayofanana na ngao,

Inachokitofautisha kigao na ngao ni kwamba kigao ni kidogo na chepesi, rahisi kubebeka, na huwa kinafungwa mkononi, lakini ngao huwa ni kubwa na nzito kidogo.

Mara nyingi katika vita vikubwa vya zamani, askari walikuwa wanakwenda vitani na ngao kubwa kwasababu vita vile, vilikuwa ni vya wengi, na mishale, mingi ilirushwa kutoka kila mahali, hivyo  palihitajika kifaa kikubwa kidogo cha kujilinda, hapo ndipo ngao ilibebwa.

Lakini katika hali ya kawaida si kila mahali askari walitembea na ngao kubwa, hivyo walibeba vigao vyepesi na umuhimu wake ulikuwa ni pale, walipojikuta katika vita vya mtu na mtu, vya kurushiana mapanga, hapo kigao kilikutumika, kupangua mapanga na sio ngao, kwasababu  ngao ni nzito, mahususi kwa kuzuia mishale ya mbali, lakini kwa vita vya mtu na mtu ni ngumu, kidogo ilihitaji kifaa chepesi..Ndio hicho kilichojulikana kama kigao.

Tazama picha juu..

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia;

Zaburi 35:1 “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.

2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie”.  

Zaburi 91:3 “Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana”,

Soma pia,

1Wafalme 10:17, 2Nyakati 9:16

Je! Kigao kinafunua nini kwa agano jipya?

Sisi kama watakatifu Bwana anatushauri, tuvae silaha zote za haki ili tuweze kuzipinga hila za shetani (Waefeso 6:11). Na moja ya silaha hizo zilizozungumziwa hapo ni Ngao., Ikimaanisha na kigao.

ngao na kigao

Ambayo biblia inasema, ndio IMANI. Hivyo Imani yetu inapaswa isimame katika vita vikubwa, na katika vita vidogo, katika mapambano makubwa na katika mapambano madogo, tushike NGAO NA KIGAO.

Yeremia 46:3 “Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana”.

Mara nyingi tunadhani shetani atatuangusha kwa mamilioni ya majeshi ya mapepo atakayotutumia.. Lakini, anaweza kutumia askari wake mmoja wa giza akatuondolea Imani yetu kwa Bwana kabisa, akaturudisha nyuma.

Hivyo ni kuwa makini, tuwe na Ngao Pamoja na vigao vyetu rohoni. Imani yetu ithibitike kotekote. Kwasababu Imani ni kitu cha msingi sana kukilinda. Na hiyo tumeambiwa tuishindanie kwasababu tumekabidhiwa tu MARA MOJA tukiipoteza basi kuipata tena ni ngumu..

Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.

Ndugu kama umeokoka, shikilia wokovu kwa nguvu zote, usirudishwe nyuma na mwanadamu mmoja au majeshi ya maadui. Simama imara na Bwana atakusaidia.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi

Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?

MJUMBE WA AGANO.

Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/02/19/kigao-ni-nini/