by Admin | 11 March 2022 08:46 am03
Dameski ni mji ambao mtume Paulo alitokewa na Bwana Yesu, wakati akiwa anaelekea kuwaua wakristo ndani ya mji huo (Matendo 9:2-7). Mji wa Dameski mpaka leo upo!.. Ni moja ya miji ambayo haijabadilika jina lake mpaka leo, mingine mfano wa hiyo ni Yerusalemu na Bethlehemu.
Mji wa Dameski upo katika nchi ya SYRIA kwasasa. Tamaduni za watu waliopo Dameski ni tofauti na za watu wa enzi za kale… Hivyo mji upo Pamoja na watu, lakini tamaduni ni nyingine si ile ya zamani.
Nabii Isaya alipewa ufunuo juu ya mji huo kuja, kuondolewa kabisa katika siku za mwisho..
Isaya 17:1 “Ufunuo juu ya Dameski. TAZAMA, DAMESKI UMEONDOLEWA USIWE MJI, NAO UTAKUWA CHUNGU YA MAGOFU.
2 Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi”.
Pia vita vya Ezekieli 38, vilivyotabiriwa kuja kupiganwa kati ya Israeli na mataifa ya kandokando Pamoja na Gogu, itaifuta kabisa mji huo.
Kwasababu kwasasa ni mji unaopinga Yerusalemu kama mji mtakatifu wa Mungu mwenyezi na urithi wa Israeli, na unafanya vita dhidi ya Taifa h. Kwasababu hiyo utaondolewa Pamoja na miji mingine baadhi kulingana na biblia.
Isaya 49:23 “Habari za Dameski. Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia; Maana wamesikia habari mbaya; Wameyeyuka kabisa; Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.
24 Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake.
25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu?
26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi.
27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi”.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/03/11/dameski-ni-wapi-kwasasa/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.