by Admin | 23 May 2022 08:46 am05
Talanta ni nini katika biblia.
Katika agano la kale Talanta kilikuwa ni kipimo cha uzito cha juu zaidi ya vyote (kilitumiwa hususani katika kupima madini ya dhahabu na fedha)..Talanta moja ina uzito wa Kg 34.2.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi..
Kutoka 25:39, 38:25, Samweli 12:30, 1Wafalme 10:10.
Lakini katika agano jipya haikutumika tu kama kipimo cha uzito bali pia kama cha fedha.
Ambapo biblia inatuambia..Talanta 1 ilikuwa na thamani ya sh5,000 ya wakati ule.
Hivyo kulingana na mfano ule wa yule mtumwa ambaye alisamehewa deni lake lililokuwa kubwa sana la talanta 10,000, ambayo tukiibadili katika pesa ya sasa si chini ya Tsh. Bilioni 6…Tunaona yeye akashindwa kumsaheme mdeni wake aliyekuwa na deni dogo..la Tsh. Laki 1.
Kama tunavyosoma habari Matokeo yake ikawa ni kukamatwa na kwenda kutupwa gerezani kwa watesaji. (Mathayo 18: 21-35)
Mfano mwingine ni habari ya yule mtu aliyesafiri, kisha akawaita watumwa wake na kuwapa talanta wafanyie biashara.mmoja akampa tano, mwingine mbili, mwingine moja. (Mathayo 25:14-30)
Hivyo katika vipimo vyote viwe ni vya kifedha au vya kiuzito bado ni vipimo vikubwa na vya juu sana.
Lakini tunaona jambo lingine katika kitabu cha Ufunuo..juu ya ile ghadhabu ya Mungu atakayoishusha juu ya dunia nzima siku za mwisho.
Anasema mawe yatakayoporomoka kutoka mbinguni yatakuwa ni makubwa kama talanta..Tengeneza picha jiwe moja lenye uzito wa kg 34.2 linaanguka juu yako ..ni mawe yenye uwezo wa kuvunja fuvu la kichwa..
Ufunuo wa Yohana 16:20-21
[20]Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
[21]Na mvua ya mawe kubwa sana, ya MAWE MAZITO KAMA TALANTA, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Si ajabu watu wataomba wafe haraka..Ili tu kujisitiri na hiyo ghadhabu kali ya Mungu mwenyezi juu ya waovu wote.
Ufunuo wa Yohana 6:14-17
[14]Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
[15]Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
[16]wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
[17]Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Ni mambo ya kutisha sana yanayokuja huko mbeleni
Jiulize unyakuo ukikupita leo, tumaini lako litakuwa ni nini… Ni majuto na vilio vya kusaga meno, ukijua kabisa hata baada ya kufa huko kwa mateso, ni safari ya moja kwa moja hadi kuzimu.
Ni heri ukampa Kristo maisha yako leo maadamu neema ipo..Unyakuo ni wakati wowote, usipumabazwe na huu ulimwengu…achana nao kwasababu Bwana Yesu anasema siku hiyo wao itawajia kwa ghafla tuwala hawatatambua lolote kwasababu wapo gizani..Na sisi tusiwe kama wao gizani ..dalili zote zimeshatimia, tunachosubiria hapa ni unyakuo basi! Hakuna mtu asiyejua hilo. Injili tuliyonayo sio ya kubembelezewa tena wokovu, ni kujionea hali halisi na kuamka usingizini mwenyewe ..
Tengeneza taa yako. Maanisha kuishi maisha wokovu, kwasababu watakaoachwa pia ni wale wanawali wapumbavu, wakristo vuguvugu (Mathayo 25).
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.
Ratli/ Ratili ni nini katika biblia?
KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.
HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU
Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/05/23/talanta-ni-nini-katika-biblia-mathayo-2514-30/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.