Nini maana ya wokovu watoka kwa Wayahudi? (Yohana 4:22)

by Admin | 27 July 2022 08:46 am07

Swali: Bwana alimaanisha nini kusema wokovu watoka kwa Wayahudi?, kwani si tunajua Wokovu unatoka kwa Mungu, iweje hapo aseme unatoka kwa Wayahudi?

Jibu: Tusome,

Yohana 4:22 “Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.”

Wokovu unaozungumziwa hapo, ni “Wokovu wa Roho”..na si wokovu wa vita au kitu kingine!, na aliposema kuwa “unatoka kwa Wayahudi” hakumaanisha kuwa Wayahudi ndio wanaoutoa wokovu na kuwapatia wengine la!, hakuna mtu wala Taifa linaloweza kuiokoa roho ya mtu!!, bali alimaanisha kuwa “wokovu unaanzia kwa wayahudi”, na ndipo unaenda kwa wengine…(yaani kwa watu wa mataifa ikiwemo na wasamaria ndani yake).

Ndio maana utaona ni kwanini Bwana wetu Yesu hakuzaliwa nje na jamii ya Israeli, wala hakuzaliwa katika Samaria, au katika Taifa lingine lolote tofauti na Israeli, badala yake alizaliwa Israeli, sawasawa na unabii Mungu alioutoa kupitia manabii wake wa zamani kama Musa, Daudi, na wengineo.

Na baada ya kuzaliwa katika jamii ya Wayahudi (yaani waisraeli), hakuanza kuhubiri injili yake kwa jamii ya watu watu wa mataifa, halafu ndio afuate kwa watu wa jamii ya Israeli(wayahudi) bali badala yake alianza kwanza kwa Wayahudi, na walipokataa ndipo akaruhusu injili ihubiriwe pia kwa watu wa mataifa ambao ndani yake pia wapo wasamaria.

Mathayo 10:5 “Hao Thenashara Yesu aliwatuma, AKAWAAGIZA, AKISEMA, KATIKA NJIA YA MATAIFA MSIENDE, WALA KATIKA MJI WO WOTE WA WASAMARIA MSIINGIE.

6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Umeona?..Wanafunzi walikatazwa na Bwana kuhubiri kwa watu wa Mataifa katika mwanzo wa Injili, lakini baadaye, baada ya Wayahudi kushiba, na kukinai….Bwana Yesu aliwaruhusu pia wanafunzi wake waende kwa watu wa mataifa duniani kote wakahubiri injili kwa kila kiumbe.

Marko 16:14 “Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.

15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Tunazidi kulithibitisha hili pia, kipindi Mtume Paulo anawahubiria wayahudi wa Antioko..

Matendo 13:45 “Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.

46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa LAZIMA NENO LA MUNGU LINENWE KWENU KWANZA; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini”.

Umeona?.. Wokovu umeanzia kwa Wahayudi, na ukaenda kwa watu wa Mataifa. Hiyo ndio sababu ya Bwana Yesu kusema.. “Yohana 4: 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.”

Je umeupokea Wokovu wa Bwana Yesu ambao tumeletewa sisi watu wa mataifa, ambao hapo kwanza hatukustahili?. Kama bado unasubiri nini?.. Pengine kweli umeupata Wokovu, lakini je! Unaujali kwa kuutunza?.. Au ni kama tu utambulisho katika Maisha yako, lakini hauna thamani nyingine yoyote ya ziada katika Maisha yako?.

Kumbuka kama unavaa nusu uchi, au nguo ambazo si za kujisitiri, kama vile suruali(kwako wewe mwanamke) au vimini tambua kuwa unaudharau wokovu wa Bwana, kama unalewa, au unacheza kamari, au unazini, au unafanya uchawi, au unaiba baada ya kuisikia injili mara nyingi, au baada ya kubatizwa..tambua kuwa unaudharau wokovu wa Bwana.

Hatari ya kutouthamini Wokovu wa Bwana ni hii tunayoisoma katika Waebrania 2:1.

Waebrania 2:1 “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.

2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

3 SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”

Utapataje kupona, wewe ambaye huujali Msalaba?..siku ile utakuwa mgeni wan ani?..ni heri ukatengeneza mambo yako leo ili uwe na uhakika wa maisha yako ya umilele.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?

USIMPE NGUVU SHETANI.

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

Mataifa ni nini katika Biblia?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/07/27/nini-maana-ya-wokovu-watoka-kwa-wayahudi-yohana-422/