Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu.

by Admin | 10 May 2023 08:46 pm05

SWALI: Kwanini wayahudi walimwambia Yesu kuwa hawajawahi kuwa watumwa wa mtu yeyote angali tunajua kuwa walishawahi kuwa watumwa kule Misri kwa miaka 400?


JIBU: Tusome;

Yohana 8:31  “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32  tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33  Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34  Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35  Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36  Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.

Kauli ya hawa wayahudi haikuwa kauli ya kweli bali ya uongo uliowazi, Na lengo la majibu yao halikuwa kutafakari Yesu anayoyasema bali kumpinga tu, Na ndio maana hawakuona shida kuzungumza uongo wa wazi, kwani vitabu vyao vinaeleza walishawahi kuwa watumwa Misri,Babeli, Ashuru na sehemu kadha wa kadha walishawahi kutumikishwa na mataifa hata wakiwa katika taifa lao wenyewe.

 Lakini Yesu hakulenga utumwa wa mwilini kama wao walivyodhani, bali ule wa rohoni, wa dhambi, yaani tamaa, wivu, uongo, mawazo mabaya, hasira n.k. Mambo ambayo walikuwa hawana.Lakini kwasababu lengo lao lilikuwa ni kumpinga waliendelea bado kusema uongo hata juu yake..Kwamfano ukisoma vifungu vinavyofuata katika mazungumzo yao, ule mstari wa 48  utaona wanasema kwamba yeye ni msamaria tena ana pepo. Jambo ambalo ni uongo mwingine wa makusudi.  Kwani Walijua kabisa Yesu ni myahudi, na wazazi wake Yusufu, na ndugu zake wote wapo nao, mpaka kazi yao ya useremala waliyoifanya waliijua, tena wakamwita Rabi sehemu nyingine,  lakini kwasababu wapo kibishi wakazusha uongo na kusema yeye ni msamaria, tena mwenye pepo.

Na ndio maana Bwana Yesu katika mazungumzo hayo hayo (Mstari wa 44) akawaeleza wazi kuwa wao ni wa Baba yao ibilisi kwasababu “hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo ”. kwasababu ya uongo wao.

Hii ni kutufundisha nini?

Tuipende kweli, Kwasababu tusipolipenda Neno la Mungu, shetani atatutumia kulipinga Neno hilo hilo kwa kushuhudia habari za uongo uliowazi na wala hututaona shida, kama ilivyokuwa kwa wayahudi hawa.

Je! Umeokoka, je! Unahakika wa maisha yako ya milele baada ya kifo? Je! Unatambua  kuwa hizi ni siku za mwisho, na roho ya mpinga-Kristo inatenda kazi ndani ya watu ambao hawajaokolewa leo? Unasubiri nini usimgeukie muumba wako, tamaa za dunia zitakufikisha wapi?umefungwa Rohoni upo chini ya Utumwa wa dhambi, anayeweza kukuweka huru ni Yesu tu peke yake. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618 / +255789001312, kwa ajili ya mwongozo huo bure.

Bwana akubariki.         

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.(

WANA WA MAJOKA.

EPUKA MUHURI WA SHETANI

YULE JOKA WA ZAMANI.

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/05/10/tu-uzao-wake-ibrahimu-wala-hatujawa-watumwa-wa-mtu/