Biblia inamaana gani inaposema tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?

by Admin | 10 August 2023 08:46 pm08

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema tutoapo unabii tutoe kwa kadiri ya imani?(Warumi 12:6)


JIBU: Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;

Warumi 12:5  Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.

6  Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7  ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8  mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

Andiko hili linatuonyesha kuwa kila mmoja wetu amepewa KIPIMO cha neema, na hicho kipimo, kwa lugha nyingine ndio kinaitwa ‘Imani’ kama ilivyotumika hapo. Maana yake ni kuwa ikiwa ni nabii, basi kuna tofauti ya viwango vya kinabii, kwamfano wapo wengine wanapewa taarifa za watu tu, wapo wengine wanapewa za nyakati zijazo, wapo wengine za mataifa, wapo wengine wanapewa taarifa dhahiri kabisa za moja kwa moja, na wapo wengine kwa njia za mafumbo n.k.. Vyote hivi vinajulikana kama ndio vipimo vya imani.

Lakini sasa ikiwa mtu hajajaliwa kuona jambo Fulani, kisha akalazimishia alione,ili tu aonekane yeye ni mwonaji wa mambo yote, maana yake mtu huyo ni kuwa amevuka kiwango cha imani alichopimiwa na Mungu.

Na hivyo ataishia kutoa taarifa za uongo ambazo Mungu hajazisema. Kwamfano mtu ataona maono, kisha asiyaelewe, hata baada ya kuomba hajayaelewa, lakini kwasababu hataki kushirikisha wenye karama za Hekima na Maarifa na upambanuzi, atataka yeye ndio atafsiri alichoonyeshwa, hivyo anatumia akili zake, na matokeo yake inakuwa ni upotoshaji badala ya ujengaji.

Vivyo hivyo na katika karama nyingine. Utakutana na mtu sio mwalimu, hajajaliwa karama hiyo, lakini kwasababu na yeye anataka kujionyesha ni mjuaji anafahamu yote, ataanza kufundisha, na hatimaye kuwapotosha watu kwa mafundisho yake dhaifu.

Mitume japokuwa walijaliwa wingi wa karama na vipawa vya Roho lakini hawakuwa hivyo. Paulo anasema..

2Wakorintho 10:12  “Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili.

13  Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu.

14  Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo;

Palepale ulipofikishwa na Bwana dumu hapo hapo, ikiwa Bwana atakuongezea neema basi itathibitika, lakini usijiongezee chochote, zaidi ya kile ulichopimiwa. Na hatari sana

Waefeso 4:7  Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo

Bwana akubariki.

 Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?

UPO UMUHIMU MKUBWA WA KUMTOLEA BWANA!

USIJISIFIE KARAMA KWA UONGO.

Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;

KUWA WEWE.

Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/08/10/tutoapo-unabii-tutoe-kwa-kadiri-ya-imani/