KUWA WEWE.

KUWA WEWE.

Shalom, Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Neno la Mungu..Ni muhimu kila mmoja wetu kuzaliwa mara ya pili na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu ni kutufanya sisi kuwa watakatifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyo mtakatifu..(1Petro 1:16).

Na kazi nyingine ya Roho Mtakatifu juu yetu ni kututumia sisi kuwavuta wengine kwa Kristo, na anaposhuka juu ya mtu anampa kipawa au karama…Karama hiyo ndiyo inayomtofautisha yeye na watu wengine..Haiwezekani watu wawili wakawa wanafanana asilimia mia..wanaweza kukaribiana huduma au karama lakini wasifanane asilimia mia. Hivyo ni muhimu sana kutojilinganisha na mwingine, wala kutotamani kuwa kama mwingine..

Kwamfano hebu tuichunguze karama ya kinabii kwa kujifunza juu ya manabii wa Bwana waliowahi kupita katika agano la kale….Tujifunze juu ya hawa manabii watatu MUSA, DANIELI na ISAYA.

Hawa watatu walikuwa ni manabii wa Bwana…na biblia inawaita wote ni manabii lakini kama ukichunguza kwa makini utaona kila mmoja alikuwa ni nabii kwa namna yake.

Tukianza na Musa, huyu hakuwa anaona maono ya siku za Mwisho, hakuwa anaona mambo yatakayokuja kutokea katika siku za mwisho kama vile siku ya Bwana, au hukumu ya mwisho wa dunia, hukumu ya wanadamu n.k Lakini Roho wa Mungu ajimtia mafuta mahususi kumfunulia torati, sheria ya Mungu, sheria za makuhani, na kumfahamisha yale yaliyotokea zamani..na alimtia mafuta kuwa kiongozi wa Taifa teule la Mungu, kuwatoa utumwani Misri na kuwapeleka nchi ya ahadi kaanani.

Lakini tukimtazama Nabii Danieli, huyu hakuwa anatembea na Mungu kama Musa…Musa alikuwa anaonana na Mungu uso kwa uso lakini Danieli hakuwa hivyo… Mungu alikuwa anamwonyesha Danieli mambo yatakayokuja kutokea siku za mwisho, kama kunyanyuka kwa mpinga Kristo, kunyanyuka kwa falme zitakazokuja kutawala dunia, kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu na kujengwa kwa hekalu..mambo ambayo Musa pamoja na uhusiano wake wote na Mungu hakuonyeshwa.

Hali kadhalika tukirudi kwa Nabii Isaya…Huyu naye hakuwa kama Musa wala Danieli…Huyu Bwana Mungu alimwonyesha zaidi mambo yajayo ambayo yatatokea baada ya mwisho wa dunia, alionyeshwa mambo yatakayotokea wakati wa utawala wa miaka 1000, alionyeshwa zaidi unabii kuhusu Ujio wa Bwana Yesu na kuzaliwa kwake kwa uwazi zaidi kuliko manabii wengine wowote..Kabla ya Nabii Isaya hakukuwa na nabii yoyote aliyejua kuwa Masihi atazaliwa na bikiri, au Bwana Yesu atasulubiwa na kuchinjwa kama mwana kondoo, wala hakuna aliyejua kwamba Masihi atapigwa kwaajili ya dhambi zetu hata Nabii Musa hakuwa analijua hilo..japokuwa alikuwa anauuona uso wa Mungu.

Hatuna muda wa kutosha wa kumwangalia Nabii Yohana Mbatizaji jinsi Roho Mtakatifu alivyomtumia tofauti na manabii wengine wote, hatujamtazama Nabii Ezekieli na Hosea jinsi Mungu alivyowatumia kama ishara..hawa walikuwa wanaambiwa waoe wake wa kizinzi, wengine wale kinyesi, wengine walala upande mmoja kwa siku nyingi..Hatujamtazama Eliya na Elisha jinsi Mungu alivyowatumia kitofauti na manabii wengine.

Eliya hakutoa unabii wowote kuhusu ujio wa Masihi, wala mwisho wa dunia lakini alitabiri mambo yaliyokuwa yanatokea papo kwa hapo..na zaidi ya yote kwa ishara na maajabu mengi..

Sasa manabii wote tuliowatazama hapo juu Biblia inawaita MANABII WA BWANA…Lakini wote hawakuwa wanafanana…Na ndio hivyo hivyo kwa Wachungaji, wainjilisti, waalimu, mitume, waimbaji, wenye karama ya Imani, wenye karama za masaidiano, wenye karama za neno la hekima na maarifa n.k… Wote hawafanani.

1Wakorintho 12:4 “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana”.

Hivyo tunajifunza ni muhimu kukaa kila mtu katika nafasi yake..kwasababu kamwe hatuwezi kufanana..Katika karama moja kuna utendaji kazi hata elfu moja tofauti tofauti…

Sasa tatizo linakuja ni mtu kutamani kuwa kama mwingine, …Unapotamani kuwa kama mwingine vilevile, ni uthibitisho tosha wa kuiua karama iliyopo ndani yako, Kwasababu kamwe hatuwezi kufanana..hata wale mapacha wanaofanana sana ukizidi kuwachunguza utaona wanao tofauti..na unavyozidi kukaa nao ndio kabisa utaona wanatofautiana sana…hiyo ikionyesha kwamba katika nafasi zetu sisi wanadamu Mungu hajawahi kutuumba tukafanana asilimia mia kama vile sisimizi wanavyofanana..

Hivyo karama Mungu aliyoiweka ndani yako ni ya kipekee tofauti na ya mwingine, na Roho ameiweka ndani yako kwa makusudi yake ya kuwavuta wengine kwake. Hivyo tembea katika kile Mungu alichokiweka ndani yako.

Bwana atusaidie sana kuzifahamu na kuzithibitisha karama zetu ili tusimzimishe Roho ndani yetu…

Maran atha!


Mada Nyinginezo:

UFANYE NINI KAMA MKRISTO WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA?

MAONO YA NABII AMOSI.

Je! Ule mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo ulikuwa ni nini?

KUMBUKUMBU LA DHAMBI.

Je ni kweli huwezi kuijua karama yako mpaka uwekewe mikono na wazee?

USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments