Je ni lazima nibadili jina baada ya kuokoka?

by Admin | 24 August 2023 08:46 pm08

SWALI: Je ni lazima nibadili jina baada ya kuokoka, na kama ni hivyo ni mazingira gani yaliyo sahihi kufanya hivyo?


JIBU: Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo.

Unapookoka, ni vema kufahamu Kristo akishakukomboa umekombolewa kweli kweli, Huwezi kukosa mbingu kwasababu ya jina lako, hata kama lina maana mbaya, kwasababu wapo watu waliokuwa na majina mabaya, mmojawapo ni Yabesi ambaye jina lake lilimaanisha “huzuni”, kwasababu alizaliwa katika kipindi cha huzuni, na wazazi wake wakamwita hivyo lakini alimlingana na Mungu na Mungu akambariki na kumtukuza sana (1Nyakati 4:9-10).Lakini walikuwepo pia watu wenye majina mazuri mmojawapo Yuda, lakini tabia zake hazikuendana na jina lake.

Hivyo ikiwa jina lako si zuri sana, na huoni shida kuendelea nalo, huwezi kumkosa Mungu kwasababu ya hilo. Lakini pia, yapo mazingira ambayo, inampasa mkristo abadili jina endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo. Na mazingira yenyewe ni kama haya;

  1. Umefunuliwa na Mungu mwenyewe: Wakati mwingine Mungu anaamua kumwambia mtu abadili jina, sio kwasababu jina lile ni baya, hapana, bali kwasababu ya kusudi alilowekewa mbele yake kulifanya. Kwamfano Mungu alimbadili jina Abramu, akamwita Ibrahimu, na tafsiri yake ni ‘Baba wa mataifa mengi’, hivyo huduma yake ya kuwa baba wa wengi, ilimpasa iendane na jina lake. Na ndivyo  ilivyokuwa kwa Sara na baadhi ya mitume.
  2. Jina lenye tafsiri ya imani nyingine/ au miungu: Yapo majina ambayo, ukiitwa mtu atatambua wewe ni wa dini nyingine, sasa hapa ni amani tu ya Kristo itawale ndani yako, ukiona ni vema ubadili, ni sawa, ili injili au ushuhuda wako usiwe na kikwazo kwa wengine mbeleni. Lakini bado hilo halikufanyi Mungu asikutumie, utatumiwa tu. Katika biblia tunaona Danieli, aliitwa jina la kipagani na Nebukadreza, Belteshaza (Danieli 1:7), Lakini hakuling’ang’ania hili jina, badala yake aliendelea kujiita Danieli, na mbingu pia ilimtambua hivyo. Japokuwa mfalme alimuita Belteshaza kufuatana na jina la miungu yake. Kwahiyo ikiwa jina lako halikaribiani na imani, ukiona vema kubadilisha hutendi dhambi.
  3. Maisha mapya:  Wakati mwingine historia yako ya nyuma, inaacha sifa mbaya katika jina lako. Kwamfano, ulikuwa ni mtu jambazi na mwizi, na unajulikana kwenye jamii kama ‘Yule Fulani kibaka’. Sasa wengi wanapookoka, wanasukumwa kabisa kubadilisha na majina yao, wawe wapya kote kote. Mfano mmojawapo wa hawa ni mtume Paulo, alikuwa mwuaji, na alikuwa anaitwa Sauli. Lakini alipomgeukia Mungu na jina lake pia akalibadili.
  4. Jina lisilo na tafsiri nzuri: Kumbuka pia wapo wengine wanakwazwa na tafsiri za majina yao. Labda anaitwa majuto, au shida, au msiba, au masumbuko. Hivyo anapookoka anapendelea ajiite majina ya ushindi au yenye Baraka. Hivyo anayechagua hili ni vizuri zaidi.

Kwahiyo hivyo ndio vigezo vya mtu kusukumwa abadili jina. Lakini usibadili kwasababu ya shinikizo la mtu, ikiwa huoni kikwazo chochote kuitwa jina hilo lako. Kwasababu wokovu wako, hauwezi kuzuiwa na jina. Hilo ulifahamu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINA LAKO NI LA NANI?

MAANA YA MAJINA NA TAFSIRI ZAKE.

Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)

Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.

Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.

KWA WINGI WA WASHAURI HUJA WOKOVU.

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/08/24/je-ni-lazima-nibadili-jina-baada-ya-kuokoka/