Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Kuna Roho inayofuatana na Majina, katika Maandiko tunaona watu wengi sana walibadilishwa majina yao, wengine wakati wa kuanza huduma au kabla ya kuanza huduma. Ibrahimu hapo kwanza aliitwa Abramu (Mwanzo 17:5), Sarai jina lake lilibadilishwa na kuitwa Sara, Yakobo jina lake lilibadilishwa na kuitwa ISRAELI. nk Kwahiyo ni Muhimu kujua maana ya majina kabla ya kumpa mtoto jina au kabla hujajipa jina.
Angalizo: Ukimpa Mtoto jina hata kama liwe zuri au lina tafsiri nzuri kiasi gani, kama mtoto huyo hatakuzwa katika malezi ya kumcha Mungu bado atakuwa mbaya tu, na akifa ataenda Jehanamu ya moto..
Kadhalika, mtoto anaweza akawa na jina lenye tafsiri isiyo njema, lakini kama atakuzwa katika Njia sahihi, hiyo haimzuii Mungu kumtumia, na jina lake kuwepo katika kitabu cha Uzima
Kwasababu majina yaliyopo katika kile kitabu cha uzima hayajaandikwa kulingana na tafsiri, bali kulingana na matendo!! Watakuwepo wengi wenye majina mazuri katika ziwa la Moto, na watakuwepo pia wengi wasio na majina mazuri Mbinguni Kwahiyo Jina pekee halimfanyi mtu au mtoto kuwa mzuri bali malezi pia ya kumcha Mungu….Na malezi sio tu kumpeleka kanisani kila jumapili, bali pia na kumfundisha Njia za Bwana kila siku hata akiwa nyumbani! huku mzazi ukionesha kielelezo cha kumcha Mungu.
Lakini yote katika yote ni vizuri kumpatia mtoto jina lililo zuri na lenye tafsiri bora!
Hili ndio jina lenye “nguvu” kuliko majina yote, hakuna lililo juu ya hili, kwa vizazi vyote mpaka mwisho wa dunia, halitakuwepo lililo kuu zaidi ya hili maana ya jina hilo ni YEHOVA MWOKOZI, Hivyo Yesu ndiye mwokozi wa Ulimwengu. (Tafadhali; Usimpe mwanao, wala usijipe mwenyewe hili jina, kwasababu ni jina tukufu la Mwana wa Mungu)
Maana yake ni “Yehova ni mwenye Neema”..Asili ya hili jina ni kiyahudi, Yohana Mbatizaji aliitwa hili jina pamoja na Yohana Mwanafunzi wa Yesu, ambaye ni ndugu yake Andrea.
Maana yake ni “Mlukania” Lukania ni mahali palipokuwa kusini mwa Italy..ambapo tafsiri yake haijajulikana mpaka leo.
Tafsiri yake ni “Zawadi ya YEHOVA” Asili yake ni lugha ya Kiebrania
Maana yake ni “Mnyenyekevu”
Maana yake ni “Yehova atapandisha au atanyanyua”..Asili ya jina hili ni lugha ya kiebrania.
Maana yake. Ni “Anayechukizwa au anayeonewa” asili yake ni lugha ya kiebrania.
Maana yake “Mungu amesikia” asili yake ni lugha ya kiebrania.
Tafsiri yake ni jiwe dogo, kama la kurusha, asili ya jina hili ni lugha ya kigiriki.
Maana ya Neema, ni upendeleo wa kipekee ambao mtu au kitu kinaweza kupata, upendeleo huo hauna chanzo/sababu maalumu. Mungu pekee ndiye anayetoa Neema.
Tafsiri yake ni “Aliye Imara, Thabiti” Asili ya jina hili ni lugha ya Kiebrania, katika Biblia alionekana Ethan mtu wa hekima katika Zaburi ya 89
Ivan na Yohana ni jina moja, isipokuwa kwa Ivan limewekwa kwa lugha ya kirusi ya sasa, lakini ni hilo hilo Yohana, ambalo tafsiri yake ni “Yehova ni mwenye Neema”
Jina Charles limetokana na neno la kijerumani “karl” lenye tafsiri ya “mwanamume”.
Jina Irene limetokana na neno la kigiriki “Eirene”…lenye maana ya “AMANI”
Jina Carolina au Caroline tafsiri yake ni “Mwanamke kwa kiingereza woman”. kwa jinsia ya kiume ni Carlos, au Charles
Jina Careen ni mchanganyiko wa majina mawili (CAROLINA na IREEN). Maana ya Irene ni “Amani”, na Caroline ni “Mwanamke”. Kwahiyo tafsiri yake ni “Mwanamke wa Amani”
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
[embedyt] https://www.youtube.com/embed?listType=playlist&list=PLIIhnDzXkeEcXSNPlq09Q5yonU3MOLI0h&v=DWFSX1GfuC8&layout=gallery[/embedyt]
About the author