KUACHA KUVUTA SIGARA.

KUACHA KUVUTA SIGARA.

Unaweza ukawa umezunguka huku na huko, umejaribu hiki na kile kwa bidii zako ili kuacha kuvuta sigara lakini imeshindikana, ni uwazi usiopingika kwamba vitu vyote vyenye addiction (yaani ulevi ndani yake) ni ngumu sana kuviacha, sio pombe, sio ugoro, sio bangi, sio madawa ya kulevya sio sigara, sio mirungi vyote hivyo kwa bidii za mtu binafsi ni ngumu leo anaweza akaacha kwa muda tu lakini kikipita kipindi Fulani kifupi ile hamu ikimzidia anarudia tena , Ni utumwa mgumu sana ambao kwa bidii za kibinadamu ni kama haiwezekani, ..Lakini nataka leo nikupe habari njema nazo ni hizi:

Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.(Yohana 8:36).  

Mamia kwa mamia kama sio maelfu kwa maelfu ya watu duniani wanaacha kuvuta sigara, kwa kumruhusu tu YESU atende kazi maishani mwao. Sio tu kwa wavuta sigara bali pia hata na kwako wewe mnywaji pombe na mtumiaji wa ugoro na madawa ya kulevya, Kwasababu kwake yeye hakuna linaloshindikana, akikufungua habakishi hata chembe moja ndani yako, haijalishi wewe ni mtumwa wa hicho kitu kwa kiwango gani, hakuna utumwa ulio mkubwa zaidi ya utumwa wa DHAMBI lakini huo aliukomesha pale msalabani, si zaidi sigara ambayo ni kitawi kidogo sana cha dhambi yenyewe?.

Ikiwa umekusudia kweli na unataka kuacha leo basi, tiba ipo kwa YESU, Hatuhitaji kusema maneno mengi  Unachopaswa kufanya ni kuanzia sasa umgeukie tu yeye..Utubu dhambi zako kwanza kwa kumaanisha kuziacha, na kisha yeye mwenyewe atakuvika huo uwezo wa kuacha kuvuta sigara, ataiondoa hiyo kiu ya sigara ndani yako moja kwa moja..Lakini Ikiwa tu umemaanisha kuwa kiumbe kipya. Kama upo tayari basi nataka ufuatishe sala hii, lakini tafuta kwanza mahali pa utulivu kisha fuatisha sala hii kwa IMANI..Kwasababu yeye yupo hapo hapo ulipo kukuhudumia hauhitaji mchungaji, au mhubiri aje kukuombea, wewe mwenyewe hapo ulipo anakusikia, kwasababu sio mchungaji anayekuponya au mhubiri bali ni yeye huyo YESU MWOKOZI ndiye anayekwenda kushughulika na shida yako…

Sema maneno haya kwa sauti:

EE! BWANA YESU, NAJA MBELE ZAKO, NINAJIJUA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEKUKOSEA KWA MAMBO MENGI, NA MOJAWAPO NDIO HILI LA KULIHARIBU HEKALU LAKO KWA KULIVUTISHA SIGARA, LEO HII NINAJUTA NA NINATUBU MBELE ZAKO KWA KUMAANISHA KABISA KUWA SITAKI KUVUTA SIGARA TENA, NA NIMEMAANISHA  KUACHANA NA MAISHA YA DHAMBI. NJOO NDANI YANGU BWANA YESU, UNIBADILISHE UNIFANYE KUWA UPYA NIFANANE NA WEWE, MIMI KWA NGUVU ZANGU NIMESHINDWA KUACHA SIGARA LAKINI WEWE ULISEMA KATIKA MATHAYO 11:28 KWAMBA TUJE KWAKO SISI WOTE TUNAOSUMBUKA NA KULEMEWA NA MIZIGO YA DHAMBI, NAWE UTATUPUMZISHA, NAWE UTATUPA RAHA NAFSINI MWETU NA LEO HII KWA UNYENYEKEVU WOTE NIMEKUJA KWAKO BWANA YESU ILI UNIFUNGUE  KATIKA VIFUNGO HIVI VYA DHAMBI NA MAUTI. NINAKIRI KUWA WEWE NDIO BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NA KWAMBA ULIKUFA NA UKAFUFUKA, NA SASA UPO HAI KUNISIKIA, HIVYO KUANZIA LEO NAAHIDI KUKUTUMIKIA NA KUKUISHIA WEWE DAIMA.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNISAMEHE NA KUNIPONYA NA SHIDA YANGU YOTE AMEN.

Ikiwa umesali sala hii kwa imani, basi fahamu kuwa Mungu amekusikia na kukusamehe dhambi zako zote sio hiyo ya sigara tu bali na nyingine zote, , hivyo unachopaswa kufanya ni kutupa sigara zote ziweke mbali nawe wakati Bwana YESU anaendelea kushughulika na hiyo kiu ya sigara ndani yako, Hivyo hakikisha, unatafuta  kanisa la kiroho, lililokaribu nawe  ili kukusaidia kukua kiroho, au wasiliana nasi kwa namba hizi 0789001312 ikiwa utahitaji msaada wetu.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

YESU NI NANI?

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

JE! KUBET NI DHAMBI?

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU.

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments