Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe?

by Admin | 17 September 2023 08:46 pm09

SWALI: Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.

JIBU:  Mstari huu una maana mbili,

Mana ya kwanza ni uhai kama ‘uhai’ alionao mwanadamu yoyote,

Maana yake ni kuwa uonapo, mtu asiyekuwa na hatia, amepangiwa njama za kuuliwa, au ndio anakaribia kufa, na wewe unaowezo wa kumsaidia huna budi kufanya hivyo wala usijifanye kama hiyo sio biashara yako.

Ni mfano wa Yule mtu aliyevamiwa na wanyang’anyi ambaye Bwana Yesu alimtolea mfano, akasema mlawi alimpomwona akapita kando, kuhani naye alipomwona akapita kando, lakini Yule msamaria akamuhurumia, akamtibu, akaokoa uhai wake. Na Yesu akasema huo ndio Upendo.(Luka 10:25-37)

Ni sawa na wakati ule Paulo amepangiwa njama na wayahudi wamvizie auawe, lakini mjomba wake alipogundua alikwenda kumjuza akida wa kikosi (Matendo 23:12-22). Huyo amemwopoa aliyekaribu na kuchinjwa.

Ni sawa na Mordekai alichofanya kwa Mfalme, Ahusuero, wale watu walipopanga njama ya kumuua akaenda kuwasemelea (Esta 6:1-12),. Ni sawa na Yonathani, alivyomtunza Daudi dhidi ya upanga wa baba yake Sauli ili asiuliwe. Hivyo hawa wote, walilitambua andiko hili, na wala hawakuogopa kutoa siri, za wale waliokusudia mabaya juu ya maisha ya wengine.

Hata leo, vifo vingi vya kikatili, vingeweza kuzuilika kwa sehemu kubwa, endapo baadhi ya wanaojua matukio hayo wangetoa taarifa mapema. Kwamfano utaona mtu anawekewa sumu kwenye chakula, wewe unayejua, ni wajibu wako kutoboa siri hiyo, ili uutunze uhai wa mtu. Utaona mwizi anapigwa, huna budi kuripoti polisi mapema maadamu jambo hilo lipo ndani ya uwezo wako, ili askari waje kumkamata wampe wao adhabu stahiki, lakini ukipita ukasema hainihusu, atachomwa moto. Lakini kumbuka uhai unathamani, hata wa mtu aliye mbaya, unathamani nyingi.

Lakini ukisema hainuhusu, Utakuwa unajipunguzia pia rehema nyingi kwa Mungu,  ndio maana mstari unaofuata unasema;

Mithali 24:11 “Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.  12 Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?”

Hivyo penda uhai, pia tunza uhai wa watu, popote pale uonapo unahatarishwa. Usiwe mzito kusaidia.

Lakini  maana ya pili ya mstari huu  ni ule Uhai wa rohoni.

Wapo watu ambao ibilisi, anakaribia kuwameza, na ukiwaacha ndani ya kipindi kifupi hakika wataangamia kabisa kiroho. Wengine wanakaribia kufa kwasababu ya huzuni mioyoni mwao, kukata tamaa, kwasababu ya dhiki na magonjwa, wengine wanakaribia kuzama katika ushirikina, wengine kwenye imani potofu ambazo zinakwenda kuwaua roho zao n.k. Hivyo makundi kama haya, unapoyaona, mwelekeo wao wewe kama mkristo uliyesimama huna budi kuwasaidia ili waokoke, wasipotelee katika mauti ya roho zao, na kwenye minaso ya adui mfano wa Yuda. Wala usisime hiyo sio shughuli yangu.

Yuda 1:22  “Wahurumieni wengine walio na shaka, 23  na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.

Hivyo tutunze Uhai, wa mwili na Roho za watu wa Mungu, naye Bwana atatunza na wetu.

Bwana akubariki

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?

Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/09/17/nini-maana-ya-mithali-2411-uwaokoe-wanaochukuliwa-ili-wauawe/