by Admin | 4 January 2024 08:46 am01
SWALI: Nini maana ya Mithali 16:30
Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.
JIBU: Mstari huo haumaanishi mtu anayefumba macho yake, Huwa anaishia kuwaza mawazo mabaya, hapana kama ni hivyo basi, tungekuwa tunafanya makosa kufumba macho tunapoomba.
Zaidi sana mtu mwenye hekima huwa anapoona jambo la kutisha ovu, au lenye aibu Ndio anayekuwa wa kwanza kufumba macho yake asiruhusu kuona kinachoendelea.. kama vile walivyofanya watoto wa Nuhu.(Mwanzo 9:23)
Hali kadhalika anaposema mtu aikazaye (aifumbaye), midomo yake. Haimaanishi mtu asiyezungumza-zungumza, Huwa anaishia kuyazungumza maneno yasiyofaa. Kama ni hivyo biblia isingesema;
Mithali 21:23
[23]Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.
Lakini je? Vifungu hivyo vilimaanisha Nini?
Hapo anaposema afumbaye macho yake ni kuwaza yaliyopotoka,..alimaanisha afumbaye macho asitazame kweli (ambayo ni Neno la Mungu), linapomfundisha au kumwonya. Mtu huyo lengo lake ni kuendelea katika mawazo yake mabaya ya dhambi. Mfano aambiwapo kuishi na mke ambaye si wako ni uzinzi, na wazinzi sehemu Yao ni Katika ziwa la moto, lakini hataki kuliona au kulisikia Hilo andiko, jibu lake ni kuwa anataka kuendelea katika matendo yake ya giza.
Ndicho kilichokuwa Kwa waliompinga Yesu., Ndio maana akasema maneno haya;
Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Vilevile anaposema “Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya”
Anamaanisha, aizuiaye midomo yake kusema maneno ya uzima, ya staha, ya kujenga, ya adabu, ya maarifa, ya busara n.k.. Mwisho wake utakuwa ni kunena maneno mabaya tu.
Bwana alisema..
Luka 6:45
[45]Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Vivyo na hivyo na sisi, hatuna budi tujipime na kujichunguza…macho yetu hutazama Nini, vinywa vyetu vimejawa na maneno gani.? Lakini fahamu kuwa huwezi kushinda jicho lako, au ulimi wako ikiwa Kristo hajaumbika ndani yako.
Je! Unataka msaada Kwa Yesu Kristo? Kama jibu ni Ndio, basi unachopaswa kufanya cha kwanza ni kuyaachilia maisha yako kwake. Ili akusamehe dhambi zako. Ndipo akupe nguvu ya kushinda dhambi.
Hivyo bofya hapa Kwa ajili ya Mwongozo wa Sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
NI WAKATI UPI UTAUONA USO WA KRISTO?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/01/04/afumbaye-macho-kusudi-lake-ni-kuwaza-yaliyopotoka/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.