Nini maana ya mmoja alikufa kwaajili ya wote hivyo walikufa wote? (2Wakorintho 5:14)?

by Admin | 22 March 2024 08:46 am03

Swali: Biblia ina maana gani inaposema, Kristo alikufa kwaajili ya wote hivyo wote walikufa?..Je na sisi tumekufa kwasababu Kristo alikufa?


Jibu: Turejee,

2Wakoritho 5:14 “Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, BASI WALIKUFA WOTE”.

Bila shaka yoyote kuwa huyu mmoja alikufa kwaajili ya wote si mwingine Zaidi ya YESU KRISTO, MFALME MKUU, BWANA wa mabwana na MWAMBA WA DAIMA!.

Lakini swali ni je!.. Kwanini afe na wengine wote wawe wamekufa?

Ni muhimu kujua kuwa wanaozungumziwa hapo kuwa “WOTE WAMEKUFA” Si watu wa ulimwengu mzima, bali ni “WALE WALIOMWAMINI YEYE”. Hao ndio waliokufa pamoja naye, maana yake mtu aliyemwamini Mwokozi YESU na kubatizwa anakuwa amekufa katika utu wa kale wa dhambi na amefufuka katika utu upya.

Wakolosai 3:3 “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu”.

Warumi 6:8 “LAKINI TUKIWA TULIKUFA PAMOJA NA KRISTO, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;

9  tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

10  Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.

11  VIVYO HIVYO NINYI NANYI JIHESABUNI KUWA WAFU KWA DHAMBI NA WALIO HAI KWA MUNGU KATIKA KRISTO YESU”.

Na hatua yote hii kwa ujumla pamoja na ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio inayoitwa KUZALIWA MARA YA PILI. Maana yake mtu anakufa katika utu wa wa dhambi na kuzaliwa katika utu upya. Na neno la Mungu linatuonya kuwa mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

Yohana 3:5“Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Je na wewe umekufa kwa habari ya dhambi kwa kuzaliwa mara ya pili?.. Kama bado basi neema ya YESU bado ipo na inakuita, ingawa haitakuwa hivyo siku zote, utafika wakati mlango wa Neema utafungwa na tumekaribia sana huo wakati, hivyo amua leo kumkabidhi YESU maisha yako kabla huo wakati haujafika, kwamaana utakapofika haitawezekana kumsogelea tena mwokozi kwaajili ya wokovu.

Luka 13:23  “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24  Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25  Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26  ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27  Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Yesu ni Mungu?, Na Kama ni Mungu kwanini alikufa?

Je Farao alikufa kwenye maji pamoja na jeshi lake au alipona?

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/03/22/nini-maana-ya-mmoja-alikufa-kwaajili-ya-wote-hivyo-walikufa-wote-2wakorintho-514/