Mathayo 6:28 “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala HAYASOKOTI
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo”
Maana ya kusokota kama inavyozungumziwa hapo ni “kitendo cha kusokota nyuzi na kuunda vazi”.
Zipo nguo/mavazi yaliyotengenezwa kwa kufuma na mengine kwa kusokota nyuzi aidha kwa mkono au mashine.
Kutoka 39:28 “na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa”
Walawi 13:52 “Naye atalichoma moto vazi hilo, kwamba ni lililofumwa au kwamba ni lililosokotwa, kama ni la sufu, au la kitani, au kitu cho chote cha ngozi, ambacho kina hilo pigo ndani yake; kwa maana, ni ukoma unaokula; vazi hilo litachomwa moto”.
Soma pia Walawi 13:58..
Sasa sisi wanadamu ili tuweze kuvaa vazi zuri lililofumwa au kusokotwa ni lazima tufanye kazi za kujiingizia kipato ili tukanunue mavazi hayo ya kusokota au sisi wenye tusokote kwa mikono yetu au mashine na kujivika…lakini kwa kawaida haiwezekani tule chakula halafu mavazi mazuri ya kusokotwa yatokee mwilini kama vile kucha inavyotokea mwilini…hilo jambo haliwezekani.
Lakini kwa upande wa MAUA ya kondeni hilo linawezekana.. yenyewe hayafanyi kazi yoyote ya kusokota lakini yanavikwa kwa rangi nzuri na za kupendeza ambazo hata Sulemani hakuwahi kuvikwa kama mojawapo ya hayo.
Kadhalika na hali yake mtu amwaminiye Bwana YESU, atakuwa hana haja ya kuhangaika sana kupata mavazi au chakula, kwasababu Bwana anajua anahitaji hayo yote.
Hata ikotokea anapitia vipindi vya kupungukiwa basi huenda ni darasa tu la muda anapitishwa lakini haitaliwa hivyo siku zote.
Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”
Kwa urefu kuhusiana na kuvikwa kwa maua ya kondeni na mfalme Sulemani fungua hapa》》》》Hii ni maana ya Mathayo 6:29 hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo
Bwana akubariki.