Vigezo na Masharti ya Mchango

HUDUMA YA WINGU LA MASHAHIDI (NURU YA UPENDO)

Tunamshukuru Mungu kwa neema yake kuu kutuwezesha kuendelea na huduma ya Wingu La Mashahidi wa Kristo. Tunawashukuru wote wanaoshiriki nasi kwa njia ya maombi na michango katika kueneza Injili na kufundisha Neno la Mungu.

Kwa kutoa mchango kupitia Wingu La Mashahidi Ministry, unakubaliana na masharti yafuatayo:

1. Madhumuni ya Michango

Michango inayotolewa kwa Wingu La Mashahidi Ministry inalenga kusaidia kazi ya huduma, ikiwemo:

  • Kuandaa na kusambaza mafundisho ya Biblia
  • Uinjilisti na kuwafikia watu kwa Injili
  • Uzalishaji wa maudhui ya Kikristo mtandaoni
  • Kuendeleza huduma za kiroho na kijamii
  • Mahitaji mengine ya uendeshaji wa huduma

2. Michango ni ya Hiari

Michango yote ni ya hiari na hutolewa kwa moyo wa ukarimu. Mchango hautoi haki ya umiliki, mamlaka, au madai maalum kwa mtoaji juu ya huduma.

3. Matumizi ya Michango

Huduma ya Wingu la Mashahidi imejitoa kutumia michango kwa uaminifu na kwa ajili ya kutimiza kusudi la huduma.

Huduma ina haki ya kupanga matumizi ya fedha kulingana na mahitaji muhimu yaliyopo ili kuendeleza kazi ya Mungu.

4. Njia za Malipo

Michango inaweza kutolewa kupitia njia rasmi za malipo zinazotolewa na huduma, ikiwemo Pesapal na njia nyingine zitakazotangazwa.Taarifa za malipo zinalindwa na mifumo ya watoa huduma wa malipo. Huduma haitunzi taarifa nyeti za kadi au akaunti za malipo.

5. Sera ya Marejesho ya Mchango

Kwa kuwa mchango ni zawadi ya hiari kwa ajili ya huduma, kwa kawaida michango haitarejeshwa.

Iwapo kutakuwa na tatizo la malipo au mchango umetumwa kimakosa, tafadhali wasiliana nasi ili jambo hilo lichunguzwe.

6. Taarifa za Watoa Michango

Taarifa utakazotoa wakati wa kuchangia, kama jina, simu, au barua pepe, zinaweza kutumika kwa:

  • Kuhifadhi kumbukumbu za michango
  • Kuwasiliana kuhusu huduma
  • Kutuma taarifa muhimu za huduma

Hatutauza wala kutoa taarifa zako kwa watu au taasisi zisizohusiana na huduma.

7. Mabadiliko ya Masharti

Wingu La Mashahidi inaweza kubadilisha masharti haya wakati wowote inapohitajika. Mabadiliko yatawekwa kwenye ukurasa huu.

8. Mawasiliano

Kwa maswali kuhusu michango, wasiliana nasi:

Wingu La Mashahidi Ministry
Tovuti: https://wingulamashahidi.org
Barua pepe: info@wingulamashahidi.org
Simu/WhatsApp: [+255 693 036 618 / +255 789 001 312]

Tunathamini ushirikiano wako katika kuendeleza kazi ya Mungu.

Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
2 Wakorintho 9:7