Biblia inaposema”Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi(Mdo 10:15)”. Je kauli hii inatupa uhalali wa kula kila kitu?

by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Kauli hiyo ilitoka kwa Mungu mara baada ya Petro kupewa maono yale ya lile shuka kubwa lililoshuka kutoka mbinguni likiwa limebeba viumbe vya kila aina najisi na safi akaambiwa avichinje ale,.Lakini Petro saa hiyo hiyo akamjibu Mungu akamwambia Mungu sijawahi kula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi katika maisha yangu yote..Ndipo Mungu akamwambia “Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi”. Ufunuo huo japo Petro alipewa kumaanisha sisi watu wa mataifa ambao hapo kwanza tulikuwa tunaonekana najisi mbele ya waisraeli, lakini Bwana alipokuja alitutakasa wote kwa damu yake hivyo sisi watu wa mataifa sio najisi tena….na hivyo Mungu hawezi kuwatakasa wanadamu walio chanzo cha uovu wote asiwatakase Wanyama ambao sio wao waliofanya makosa, kwahivyo Wanyama nao wametakaswa hakuna kilicho najisi tena….

Kwahiyo ono lile Petro aliloonyeshwa ni Ufunuo mkubwa sana unaoonyesha wazi wazi kuwa mbele za Mungu hakuna kiumbe chochote kilichonajisi msalaba umefumbua hilo fumbo….Ikimaanisha kuwa viumbe vile ambavyo hapo mwanzo vilikuwa haviliwi sasa vyote vinaweza kuliwa, na sisi watu wa mataifa ambapo hapo kwanza tulikuwa hatustahili kumjua Mungu wa Israeli(tulikuwa najisi) sasa ni Taifa teule la Mungu.   Utaona jambo hilo hilo Mtume Paulo akilirudia sehemu fulani na kusema amehakikishiwa na Mungu kabisa hakuna kitu chochote kilichonajisi kwa asili yake Ukisoma

Warumi 14:14 “Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.”  

Lakini kumbuka pia kauli hiyo haijatupa ruhusa ya sisi kuwa walafi, biblia hiyo hiyo inasema japo vitu vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo kwa mtu,(1Wakoritho 6:12), Kumbuka hata wanyama wale au vyakula vile vinavyokubalika na wengi na vinavyoonekana kuwa ni safi, bado vinaweza visimfae mtu mmoja mahali Fulani, Sio wote wanapenda nyama ya samaki, si wote nyama ya ng’ombe inawakubali, si wote nyama ya kuku inawakubali, si wote maziwa yanamanufaa mwilini mwao, sasa mtu kama huyo akila na kusema kuku imekubaliwa kwenye maandiko ngoja niishambulie, baadaye ikishamsumbua anaanza kulalamika, lakini ameshindwa tu kutumia hekima kufahamu neno hili “vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo”..  

Vilevile ukila nyoka, au panya, au mjusi, au mende, kama hicho ni chakula kinachokubalika na jamii yenu na wewe pia unakipenda na hakikuletei madhara yoyote mwilini mwako, Hakuna shida yoyote kula tu hata vipepeo, na kinyonga ilimradi uvipokee kwa shukrani [yaani kwa kumaanisha](1Timotheo 4:3), Na sio kwa ulafi, kisa tu vimehalalisha vyote.

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE”?

UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?

WAPUNGA PEPO WANAOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NI WATU WA NAMNA GANI?

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.

HISTORIA YA ISRAELI.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/biblia-inaposemavilivyotakaswa-na-mungu-usiviite-wewe-najisimdo-1015-je-kauli-hii-inatupa-uhalali-wa-kula-kila-kitu/