LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

by Admin | 28 November 2019 08:46 am11

Litania ya bikira Maria mtakatifu ni nini?, Je Maria ni Malkia wa Malaika, Malkia wa mitume na malkia wa wakristo?.

Maana ya “LITANIA” ni Mfululizo wa sala ambayo maneno yake ni ya kujirudia rudia, ambayo yanahusisha upande mmoja kuitikia. (Mkusanyiko unaitikia). Mtindo huu wa sala unatumika sana na Kanisa Katoliki.

Sehemu ya baadhi ya Maneno yanayotamkwa katika sala hiyo ya litania ya bikira maria ni haya..

Lakini je! Sala hii ni ya kimaandiko?.

Kabla ya kuitafakari kama ni sala ya kimaandiko au la..Ni muhimu kufahamu kuwa lengo la ujumbe huu..sio kumshutumu mtu, wala kumhukumu, wala lengo sio kujifanya kuwa upande mmoja unajua zaidi ya mwingine..Lengo kuu ni kujifunza Maandiko, huku tukionyana na kusahihishana kasoro zetu kwa kutumia Biblia. Kama tulivyoagizwa katika Wakolosai 3:16.

Sasa tukirudi kwenye sala hiyo hapo juu..Tunaweza tukahoji mambo machache muhimu..

Je! Ni kweli  Maria Mtakatifu? na ni mama mwenye Ubikira?..

Si kweli  kwasababu Maria Baada ya kumzaa Bwana hakuendelea kuwa Bikira..na pia alipokufa, alizikwa na huko alipo sio bikira, yupo katika roho ambapo yeye naye anasubiri ufufuo ambao utakaokuja katika siku ile ya unyakuo,..ambapo atavaa mwili wa utukufu kama watakatifu wengine na kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Hivyo hawezi kuombwa kwa lolote wala haelewi kinachoendelea duniani.

Kadhalika Maria sio Malkia wa wakristo wala Malkia wa Malaika.  Kwasababu Malaika hawana Malkia,..Na hakuna mahali popote katika maandiko matakatifu panasema hivyo..Isipokuwa wapagani ndio walikuwa wanaabudu kiumbe wanachokiita wao malkia wa mbinguni. Lakini katika maandiko hakuna sehemu yoyote inayoonesha kuwa kulikuwa au kutakuwepo na malkia wa malaika. Hivyo ni dhahiri kuwa kama sala hii haipo katika Biblia basi ni lazima itakuwa imetungwa tu na watu fulani ambao nia yao ni kupoteza wengine.

Pia Maria sio Malkia wa Mitume, wala  wa manabii wala sio malkia wa mababu, wala malkia wa wakristo..

Hivyo sala hii sio sala ya kimaandiko bali ya kibinadamu, ambayo ndani yake upo mpango mkubwa sana wa Ibilisi..kuwafanya watu waabudu sanamu na vitu visivyokuwepo..

Ndugu kama unataka kusali, Bwana Yesu mwenyewe alitufundisha sala..Nayo ni hii..

Luka 11:1 “Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.

2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]

3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.

4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu]”

Ingekuwa Maria anastahili kuombwa Bwana Yesu angewafundisha wanafunzi wake hapo juu wamwombe Maria..Lakini unaona hajafanya hivyo..Ikimaanisha kuwa sala inastahili kwenda kwa Baba yetu wa Mbinguni basi.

Kama ulikuwa unasali sala hiyo ya “litania ya bikira Maria” na hukujua kuwa ni sala ya uongo, na leo umejua. Usifanye hivyo tena, ni machukizo mbele za Mungu..Ni ibada za sanamu ambazo Mungu amezikataza mara nyingi katika Biblia..Mpe leo Yesu Kristo maisha yako naye atakupa tumaini na moyo mpya wa sala..

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/11/28/litania-ya-bikira-maria-je-ni-sala-ya-kimaandiko/