Je! Lewiathani ni nani?

by Admin | 16 July 2020 08:46 pm07

Lewiathani ni nani?


Zaburi 104: 25 “Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.

26 Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo LEWIATHANI ULIYEMWUMBA ACHEZE HUMO.

27 Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake”

Vipo viumbe vingi vilivyopo ambavyo havijagunduliwa bado, na pia vipo baadhi ambavyo vilipotea wakati wa gharaka…tafiti zinaonyesha kuna idadi kubwa sana ya viumbe vinavyopotea kila siku duniani, inakadiriwa kuwa kati ya aina 200-2,000 ya viumbe vinapotea kila mwaka ulimwenguni ambayo ni idadi kubwa sana, na vipo pia ambavyo vinagunduliwa, ambavyo vilikuwa havijawahi kufahamika.

Sasa kama biblia inavyosema hapo juu kuna nyoka baharini aitwaye “lewiathani”..Huyo nyoka ni kweli yupo…Ni aina ya nyoka tu ambao pengine wanaweza kuwa wakubwa zaidi kuliko nyoka wa kawaida kama chatu au anakonda na wenye uwezo mkubwa, lakini wamo humo baharini, na Wanasayansi bado hawajawaona, lakini labda watakuja kuwaona au walishatoweka zamani kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi…lakini watu walioishi zamani waliwajua nyoka hao kiundani.

Lakini hilo sio la muhimu sana, kufahamu kama wapo au la!…na wala si suala la kuweka hofu, kwamba kitakuwa ni kiumbe cha kutisha sana na cha kuogopeka…Kwasababu viumbe vyote vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu vimewekwa chini ya Mwanadamu, avitiishe na kuvitawala, hakuna kiumbe chochote kilichomzidi mwanadamu kwa uweza na nguvu…Hivyo hata vikiwa na umbo kubwa na la kutisha kiasi gani, bado havitakuwa na akili kama mwanadamu, na vitakuwa chini ya mwanadamu tu!…haijalishi vitakuwa vimesifiwa kiasi gani katika biblia, bado havitakuwa na utashi wala akili ya kumzidi mwanadamu..

Kwamfano utaona katika biblia wanyama wengine wakisifiwa sana (Ayubu 40:16-24, na Ayubu 41:12-34), lakini bado haviwezi kulinganishwa na mtu.

Na huyu Nyoka anayeitwa LEWIATHANI ni hivyo hivyo..ni mnyama tu kama wanyama wengine, haijalishi atasifiwa kiasi gani lakini bado atakuwa ni mnyama tu atakayekuwa chini ya mwanadamu.

Ayubu 3:7 “Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.

8 Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani”.

Sasa kwanini biblia imtaje huyu Lewiathani?.

Biblia mara nyingi inatumia Wanyama kuwafananisha na watu…kwamfano utaona shetani anatambulika kama JOKA (Ufu.12), kutokana na mnyama wa kwanza kukaribisha dhambi ulimwenguni kuwa “nyoka”..hali kadhalika Bwana wetu Yesu anafahamika kama “mwanakondoo” kutokana na tabia ya upole wa kondoo n.k

Hivyo pia Lewiathani kama nyoka aishie baharini tabia zake zimefananishwa na tabia za mpinga-Kristo ambaye siku za Mwisho Bwana atamwua.

Isaya 27:1 “Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini”.

Tunasoma pia katika…

2Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;

9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”.

Siku za mwisho Bwana atamharibu mpinga-kristo na wafuasi wake wote…Bwana atusaidie kutuepusha na roho ya MpingaKristo ambayo inatenda kazi sasa.

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.

Kwanini Bwana alirejea Tiro na Sidoni kwa mfano wa Sodoma?

Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?

https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/maswali-na-majibu-2/

Nini maana ya ‘Usimwekee mtu mikono kwa haraka’?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/16/je-lewiathani-ni-nani/