Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.

Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.

Ndio yupo samaki ajulikanaye kama nguva, kwa lugha ya kiingereza anaitwa Sea cow, kwa maelezo yake marefu juu ya mwonekano wake na jinsi anavyozaa, na kuishi baharini msome Wikipedia kwa link hii>> https://sw.wikipedia.org/wiki/Nguva

Lakini huyu samaki nguva sio kama wale watu wanaomaanisha kwamba anakiwili wili cha mwanadamu na mkia wa samaki (samaki mtu).. Katika uumbaji wa Mungu hakuna kiumbe kama hicho, wala huwezi kukikuta katika bahari yoyote duniani.

Viumbe hawa walianza kuzungumziwa tangu zamani kwenye hadithi za kimila za mataifa mbali mbali,huko Asia na Ulaya lakini katika maisha halisi hawapo, wengine wanasema samaki hao wanaweza wakaongea kama mwanadamu, lakini hilo jambo ni batili.

Katika Biblia kiumbe kama huyu hajatajwa, aliyetajwa ambaye kidogo aliweza kumkaribia mwanadamu ni NYOKA peke yake, Na hiyo ilikuwa ni kabla hajalaaniwa(Mwanzo 3:1)..Yeye ndiye aliyekuwa mwerevu kuliko wanyama wote mwituni, aliweza kuongea kama mtu, na alikuwa anatembea kwa miguu, lakini alipolaaniwa ndio akawa nyoka huyu ambaye tunayomwona sasa, anatembea kwa matumbo, hata akili yoyote.

Kwahiyo baada ya hapo hakukuwa na kiumbe mwingine yeyote aliyemkaribia mwanadamu.

Lakini pia ni vizuri kufahamu, mambo mengi sana ya ki-pepo, yanahushishwa na hivi viumbe vya kudhaniwa wasio halisi.. kwamfano Dragoni, joka lenye vichwa saba litoalo moto mdomoni, ni mungu wa jamii Fulani huko Asia, hususani China, ambaye kiuhalisia nyoka huyo hayupo duniani, fuatilia tena tembo mwenye mikono mingi huko India, samaki mtu, n.k.

Hivyo kuwa makini na elimu kama hizo, ni rahisi kushawishiwa kuwa viumbe kama hao wapo, na kupewa maelekezo jinsi ya kuwaona au kukutana nao, kumbe hujui ndivyo unavyoingizwa katika elimu za mashetani na mwisho wa siku unazama kabisa huko, unadhani umefanikiwa kuwaona kumbe ni mapepo yaliyojigeuza kwa mfano wa hivyo viumbe visivyo halisi..

Hizi ni siku za mwisho za hatari biblia inasema..

1 Timotheo 4 :1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”

Unaona? Mafundisho ya mashetani yamezaa kila kona..Na kama husomi biblia yako, basi upo hatarini kuchukuliwa nayo moja kwa moja..Je! Umempa Yesu maisha yako? Kama sivyo unasubiri nini, huoni kama upo hatarini? Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho. Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwake, na yeye ni mwaminifu atakuokoa na kukusamehe makosa yako yote, haijalishi ulifanya dhambi kiasi gani.

Ubarikiwe.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

 

MAFUNDISHO YA MASHETANI

NAO WATAKAOUAWA NA BWANA WATAKUWA WENGI.

ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.

PARAPANDA ITALIA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Paul
Michael Paul
9 months ago

Barikiwa kwa somo zuri.