Neno la Mungu la leo.

by Admin | 24 July 2020 08:46 pm07

Neno la Mungu la leo ni lipi?


Kwanza nakupongeza kwa kupenda kutafuta kujua Neno la Mungu la leo..

Bwana Yesu alisema kila atafutaye huona (Mathayo 7:8), Hivyo kwa kuwa na wewe umetafuta kujua Neno la Mungu la leo kwako, basi ni hakika kuwa lipo jambo jipya Mungu atakufundisha.

Sio kwa bahati mbaya umefika mahali hapa.,

Paulo alimwambia Timotheo.

1Timotheo 4:13 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma…..”

Unaona ni jukumu la kila mmoja wetu kuonyesha bidii katika kusoma(kujifunza) Neno la Mungu.

Wewe unaonyesha bidii hiyo  hivyo, usiache kupitia somo hili mpaka mwisho, lipo ambalo Mungu amekuandalia leo..

Lakini kabla hatujaendelea unaweza kufungua hapa  uingie katika horodha ya masomo ya kujifunza yaliyotangulia zaidi ya 1000, pamoja na maswali na majibu ..

>>> MAFUNDISHO MAPYA.


Leo tutajifunza nini maana ya Upendo na je! kuna aina ngapi za upendo?

Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha matokeo chanya, aidha umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye.

Kuna aina kuu tatu za upendo.

  1. Upendo unaotokana na Hisia, (Eros), Mfano wa upendo huu ni mke na mume. Sulemani aliutaja upendo huu sana katika kitabu cha Wimbo ulio bora (Wimbo 1:13-17)
  2. Upendo unatokana na  mahusiano mtu mmoja aliyo nayo kwa mwingine.(Phileo). Kwamfano unaweza ukawa unampenda mtu kutokana na kwamba ni mchezaji mwezako, au mfanyakazi mwenzako, au mkristo mwenzako, au mwanafunzi mwenzako n.k. mazingira yakishawatawanyisha, au itikidi zikitofautiana basi Upendo huu unakufa.
  3. Upendo wa ki-Mungu (Agape). Upendo huu ndio Upendo mkuu kuliko yote, Ni upendo usiokuwa na Masharti, Ni upendo ambao mtu anakupenda sio kwasababu ulimfanyia hiki au kile, au kwasababu unaendana naye kitu Fulani, hapana..Ni upendo usiohesabu mazuri wala mabaya kama kigezo cha kukupenda, ..

Upendo huu ndio ule ambao Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).

 Na Upendo aliokuwa nao Yesu, ukamfanya mpaka auote uhai wake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi. Upendo wa namna hii ukiwa nao basi ujue kuwa Upo karibu na Mungu sana kuliko mwanadamu mwingine yeyote duniani.

Na unamjua Mungu, zaidi mwanadamu mwingine yoyote duniani haijalishi atasema anaona maono, au ana mafunuo mengi kiasi gani..

1Yohana 4:7 “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo”.

Tabia za upendo huu unaweza kuzisoma katika kitabu cha 1Wakorintho 13:4-8

Kwa urefu wa maelezo haya juu ya aina hizi za upendo fungua hapa usome..>> UPENDO

Hivyo hiyo yote ni kuonyesha jinsi gani Mungu anatupenda na kutujali, Hivyo kama wewe ni mwenye dhambi ujue kuwa Mungu anakupenda bado na hivyo hataki upotee, uende kuzimu, mgeukie leo akuoshe dhambi zako. Ili ukaurithi uzima wa milele aliotuandalia. Hilo ndilo Neno la Mungu la leo.

Shalom.

Tazama vichwa vingine vya masomo chini, kwa maarifa zaidi ya kiroho.

Mada Nyinginezo:

RABI, UNAKAA WAPI?

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/24/neno-la-mungu-la-leo/