Rangi ya kaharabu ni ipi kibiblia(Ezekieli 1:4,27,8:2)?

by Admin | 24 September 2020 08:46 pm09

Rangi ya kaharabani ni ipi?


Rangi ya kaharabu ni rangi iliyo katikati ya Njano na machungwa, kwa lugha rahisi ya kueleweka wengi wanaiita Njano, japo si njano kabisa. Tazama picha.

Hivi ni vifungu katika biblia vinavyoizungumzia rangi hiyo;

Ezekieli 1:4 “Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo”.

Ezekieli 1:27 “Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote”.

Ezekieli 8:2 “Ndipo nikaangalia, na tazama, kana kwamba ni mfano wa moto; tangu mfano wa viuno vyake na chini, moto; na tangu mfano wa viuno vyake na juu, kana kwamba ni mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu”.

kaharabu

Ukuu na uweza wa Mungu umeonekana kwa rangi hii, Na ndio maana utaona karibu vifungu vyote, ambapo Mungu anaanza kujidhirisha mbele ya watu rangi hii au moto unatajwa. Kuashiria kuwa yeye ni kama Moto, unaosafisha fedha, na kuteketeza makapi.

Waebrania 12:29 “maana Mungu wetu ni moto ulao”.

Hivyo ni jukumu letu sisi kufanyika mawe ya thamani mbele za Mungu kama fedha na dhahabu ili apitapo juu yetu atusafishe zaidi badala ya kututeketeza, lakini tukiwa kama nyasi tu mbele zake, (mapaki), yaani watu waovu wasiomcha Mungu, watenda mabaya, ni wazi kuwa akipita juu yetu tutateketea kwasababu sisi ni mapaki tu..Na ndicho kinachowakuta watu wengi siku ile ya mwisho.

Mathayo 3:12 “……bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.

Bwana atusaidie.

Shalom.

Tazama maana nyingine za maneno chini, na masomo yake.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

MAANA YA RANGI KIBIBLIA.

DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/24/rangi-ya-kaharabu-ni-ipi-kibiblia/