Nasaba ni nini kibiblia?(1Nyakati 9:1, Tito 3:9)

by Admin | 4 October 2020 08:46 am10

Nasaba ni nini kibiblia?


Ni mfululizo wa majina ya watu au watawala  katika ukoo mmoja, Kwamfano kitabu cha Mathayo sura ile ya kwanza kinaonyesha nasaba ya Bwana wetu Yesu Kristo (yaani ukoo wake tangu Ibrahimu mpaka kuzaliwa kwake), Na kile cha Luka sura ya tatu kuanzia mstari wa 23-38, kinaeleza ukoo wake tangu kuumbwa kwa Adamu, yaani huyu alimzaa huyu, na huyu akamzaa huyu,  hivyo hivyo mpaka vizazi vyote vipite hapo katikati. Hiyo ndio maana ya Nasaba.

Wana wa Israeli nao pia walihesabiwa kwa nasaba,

Na hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na neno hilo;

1Nyakati 9:1 “Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao”.

 

1Nyakati 5:1 “Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza”.

 

Tito 3:9 “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana”.  

 

1Timotheo 1:4 “wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si madaraka ya Mungu yaliyo katika imani; basi ufanye hivyo”.

Soma pia,

1 Nyakati 5:7, 9:22 2Nyakati 12:15, 31:16,17,19, Ezra 2:62,8:2.

Hata sisi pia tunahesabiwa kwa nasaba rohoni, pale unapomletea mmoja kwa Kristo, mbinguni inarekodi kuwa huyo ni mwana wa wako uliyemzaa kwa Bwana, na Yule uliyemzaa akakomaa akaenda kumleta mwingine kwa Kristo, anaonekana kuwa yeye ndiye aliyemzaa, hivyo hivyo, lakini chanzo ni wewe.

Na hiyo inafanya jina lako liwe kubwa katika ufalme wa mbinguni, kulingana na Nasaba yako.

Je! Na sisi tunayo juhudu katika kumzalia Mungu matunda?. Kama hatuna tunapaswa tuanze ili tujijengee daraja zuri mbinguni.

Shalom.

Tazama tafsiri ya maneno mengine chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Rangi ya kaharabu ni ipi kibiblia(Ezekieli 1:4,27,8:2)?

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

UCHAWI WA BALAAMU.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

 

MAONO YA NABII AMOSI.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/10/04/nasaba-ni-nini-kibiblia1nyakati-91-tito-39/