Chamchela ni nini kwenye biblia?(Zaburi 58:9, Amosi 1:14)

by Admin | 28 October 2020 08:46 pm10

Chamchela ni neno linalomaanisha  ‘kisulisuli’,

Utalisoma neno hilo kwenye vifungu hivi katika biblia;

Zaburi 58:9 “Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto. ”

Isaya 29:5 “Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.

6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao”.

Amosi 1:14 “lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela”;

Hivyo,Chamchela au kisulisuli ni moja ya njia ambayo Mungu aliitumia kuonyesha mambo mawili makuu. Jambo la kwanza ni ili kudhihirisha ukuu wake kwa wanadamu, na jambo la pili ni kuonyesha ghadhabu yake kwa waovu.

Kwamfano utaona alijifunua kwa Ayubu kwa njia hii pale alipotaka kumuonyesha ukuu wake na uweza wake.

Ayubu 38:1 “Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,

2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa”?

Soma pia Ayubu 40:6

Vilevile utaona pia anajidhihirisha kwa njia hii, kuonyesha ukali wa hasira yake jinsi anavyoweza kuwapeperusha waovu wasionekane kabisa kwa mfano wa kisulisuli.

Isaya 41:16 “Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli”.

Yeremia  23:19 “Tazama, tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani. 20 Hasira ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa”.

Nasi pia tunapaswa tuishi maisha yampendezayo Mungu angali tukiwa hapa duniani, ili Bwana atakapojifunua kwetu, ajifunue kwa sauti ya upole na utulivu, kama alivyofanya kwa Eliya na sio kwa Chamchela.

Shalom.

Tazama maana ya maneno mengine ya kwenye biblia chini.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Zaburi maana yake nini, katika Biblia?

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

Hori ni nini kibiblia (Waamuzi 5:17, Luka 2:7)?

Neno Bildi linamaanisha nini kwenye biblia(Matendo 27:28) ?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/10/28/chamchela-ni-nini-kwenye-bibliazaburi-589-amosi-114/