Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

by Admin | 27 November 2020 08:46 pm11

Biblia inaziorodhesha bahari kuu nne, tuzisome;

1 ) Bahari ya shamu: Kwa sasa inajulikana kama bahari nyekundu, (Kwa kiingereza red sea). Hii ni ile bahari ambayo wana wa Israeli waliivuka baada ya Mungu kuipasua pale walipokuwa wanafuatiliwa na maadui zao, ambapo tunaona baadaye walikuja kumezwa na bahari ile.

bahari ya shamu

Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji”.

2) Bahari kubwa , au bahari ya Wafilisti, (Kutoka 23:31): Kwasasa inajulikana kama habari ya Mediteranea. Ipo upande wa Magharibi wa taifa la Israeli. Hii ndio bahari kubwa kuliko zote zinazoorodheshwa kwenye biblia.

bahari kubwa, ya wafilisti, au mediterenia

Hesabu 34:6 “Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; hii ndiyo mpaka wenu upande wa magharibi”.

Soma pia Yoshua 9:1, 15:47, 23:4, Ezekieli 47:19

3) Bahari ya Galilaya; Au kwa jina lingine Bahari ya Tiberia, au ziwa la Genesareti au Bahari ya Kinerethi Yoshua 12:3, 13:27, 34:11. Hii ndio ile bahari ambayo Bwana Yesu alitembea juu ya maji.

bahari ya galilaya

Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,”

Mathayo 4:18 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi”.

4) Bahari ya chumvi: Hii ni habari ndogo sana, ambapo ipo chini ya mto Yordani, maji yake ni ya chumvi nyingi sana, jambo ambalo linaifanya bahari hiyo isiwe na kiumbe wa kuishi ndani yake kama samaki, sehemu nyingine wanaiita ‘bahari mfu’(Dead Sea)

bahari ya chumvi

 Hesabu 34:3 “ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki”;

 Kumbukumbu 3:17, Yoshua 15:2.

Shalom, tazama maeneo mengine mbalimbali ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/11/27/bahari-mbalimbali-zilizoorodheshwa-kwenye-biblia/