Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika (Isaya 6:8)

by Admin | 25 January 2021 08:46 am01

SWALI: Mtumishi wa Mungu! Bwana asifiwe, naomba ufafanuzi kidogo juu ya andiko hili katika Isaya 6:1-10 Ni Nani aliyesema “Nitume Mimi”?je Ni isaya au!? Na kwanini Isaya pia alitakaswa kwa kaa la moto?


JIBU:  Tusome baadhi ya vifungu hivyo;

Isaya 6: 5 “Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi.
6 Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;
7 akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.
8 Kisha nikaisikia SAUTI YA BWANA, AKISEMA, NIMTUME NANI, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, MIMI HAPA, NITUME MIMI.
9 Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione.
10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa”.

Shalom, Unabii huo ulikuwa unamuhusu Nabii Isaya mwenyewe aliyekiandika kitabu hicho, tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa huyo ni Yesu ndiye aliyesema maneno hayo, nitume mimi.?

Hiyo yote ni baada ya Isaya kuijiona amesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu mbinguni, na kwamba muda mfupi baadaye atahitajika kufanya mahojiano na Mungu. Hivyo kwa kulijua hilo kabla hata hajasema chochote, alijitambua hali yake ilivyo kuwa yeye ni mtu mwenye midomo michafu, akiwa na maana mwongo, msengenyaji, mtukanaji n.k. Jambo ambalo halikuwa kuwa midomoni mwa Yesu, tangu anazaliwa.

Hivyoo akaomba kwanza tiba, asafishwe kinywa chake, kabla ya kuzungumza na Mungu,  ndipo hapo utaona huyo kerubi akichukua kaa la moto kutoka katika madhabahu ya Mungu kwa koleo.. Sasa zingatia hilo neno madhabahu, kaa lile halikutolewa sehemu nyingine yoyote Zaidi ya madhabahuni pa Mungu. Na pia hakupewa kipelekewa kitu kizuri mdomoni labda tuseme embe au ndizi, au tango kimponye badala yake alipelekewa kaa la moto.

Na kama tunavyofahamu moto kazi yake ni kuunguza, tena, mbaya Zaidi pale unapokutana na mdomo, jaribu kutengeza picha kaa jekundu linakuja kugusana na midomo yako, mshituko na maumivu utakayosikia hapo yatakuwa ya namna gani, ni heri ungelikanyaga kwasababu mguu kidogo ni mgumu, kuliko kukutana na ulimi.

Lakini ndiyo njia ambayo Mungu aliichagua kumponya Isaya na midomo yake michafu.

Hata leo hii, ili Mungu aweze kutuponya na midomo ya usengenyaji, uongo, fitina, kiburi, ya faraka, n.k. Ni lazima tukubali kaa la Mungu lipitishwe vinywani mwetu.

Na kaa hilo halitoki sehemu nyingine isipokuwa madhabahuni pa pake, ikiwa hatutaki kukemewa dhambi zetu, hatutaki kukaripiwa, hatutaki kuonywa kwa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu, hatutaki kuhubiriwa maneno magumu yanayochomo mioyo yetu, ili tubadilike, kamwe, tusitegemee kama usengenyaji utaondoka vinywani mwetu.

Kama tutapenda wakati wote injili ya kupiga adui zetu, na injili za mafanikio, hatutaki kukemewa dhambi zetu, na kuelezwa uhalisia wa ziwa la moto  kamwe vinywa vyetu haziwezi kuponywa.

Hivyo tukubali kukaripiwa na Mungu, tukubali kukemewa na yeye, kwasababu kwa njia hiyo ndio kaichagua ili kutuponya sisi, hakuna short-cut, Mungu anatujua vizuri sisi wanadamu, wakati mwingine tutahitaji moto ili tuponywe.

Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?

KWANINI MIMI?

Nini maana ya uvuvio?.

UFUNUO: Mlango wa 15

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/01/25/ni-nani-aliyesema-nitume-mimiisaya-68/