Nini maana ya uvuvio?.

Nini maana ya uvuvio?.

Uvuvio ni Nini?

Neno uvuvio maana yake ni “kupuliza hewa kwa nguvu”..unapopuliza makaa ya moto maana yake unayavuvia makaa. Unaweza kuuvuvia makaa ya moto kwa mdomo au pepeo.

Ayubu 20: 26 “…..Moto ambao HAUKUVUVİWA na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake”.

Maana ya mstari huo ni kwamba, moto ambao umezuka tu wenyewe ambao haujapulizwa na mtu utaiteketeza nyumba yake.. Jambo ambalo ni kweli, kwani nyumba zote zinazoungua, ni kutokana na moto, uliojivuvia wenyewe wakati mtu huyo hayupo..kwasababu kama mwenye nyumba angekuwa ni yeye kauvuvia huo moto asingeruhusu, auvuvie mpaka uwe mwingi kiasi cha kuunguza hema yake, anguvuvia kiasi cha kutosha kupikia au kufanyia shughuli zake ndogo, na kuuzima atakapomaliza. Pia unaweza kusoma Isaya 57: 13, inazungumzia habari hiyo hiyo ya Uvuvio.

Sasa tukirudi katika Agano jipya, tunaona biblia imelifananisha tendo la kupokea Roho Mtakatifu, na uvuvio.

Yohana 20: 22  “Naye akiisha kusema hayo, AKAWAVUVİA, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu”.

Maneno hayo aliyazungumza Bwana, kama ahadi ya kitu kitakachokuja kuwatokea wanafunzi wake siku chache mbele…Na tarehe ilipofika, iliyopangwa na Mbingu ya wao kumpokea Roho Mtakatifu (yaani siku ile ya Pentekoste)..Roho aliwafikia kama UVUVİO WA UPEPO.

Maana yake ni kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu yao kama UPEPO ULİOPULİZWA.. Na kama unajua kazi ya upepo ni kuchochea moto. Kikawaida upepo unavyozidi kuwa mkali ndipo moto na wenyewe unavyozidi kuwaka na kusambaa kwa kasi na kusababisha madhara makubwa..

Matendo 2: 1  “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2  Kukaja ghafula toka mbinguni UVUMİ KAMA UVUMİ WA UPEPO WA NGUVU UKİENDA KASİ, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.

Ule upepo ulianza kuchochea, cheche ndogo iliyokuwepo ndani yao, na kufanya Moto mkubwa kuwaka ndani yao, Moto ule ulianza kukaa kwanza kwenye ndimi zao, kila mmoja akaanza kuzungumza kwa lugha mpya, na maneno yenye moto, unaounguza kila kazi za ibilisi na unaoteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo, na baadaye ukasambaa katika mwili wao wote, na kuwafanya waweze kufanya miujiza na ishara zisizo za kawaida.

Hivyo Roho Mtakatifu hata sasa yupo, Ahadi ile hawakupewa mitume pekee yao..Biblia inasema hivi..

Matendo 2:37  “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  KWA KUWA AHADİ Hİİ Nİ KWA AJİLİ YENU, NA KWA WATOTO WENU, NA KWA WATU WOTE WALİO MBALİ, NA KWA WOTE WATAKAOİTWA NA BWANA MUNGU WETU WAMJİE.

40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.

Biblia inasema hapo katika mstari wa 39, kwamba ahadi hiyo ya Roho Mtakatifu ni kwa watu wote, watakaomjia Bwana. Yaani mimi na wewe, na mtu mwingine yeyote, Sasa tunamiaje Bwana?..Biblia imetupa jibu katika huo mstari wa 38 kwamba….. “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Ndugu, inawezekana kuna kipawa Mungu kaweka ndani yako na haujijui, inawezekana kuna huduma ameweka ndani yako kwaajili ya kuujenga ufalme wake, na haujui au nguvu yako ni ndogo (ipo kama cheche tu).. Hiyo ni kwasababu UVUVIO haujapita juu yako.. moto uliopo ndani yako bado haujachochewa, lakini siku utakapochochewa ndipo utakapoona tofauti yako ya siku hizo na siku za nyuma. Kama unatamani uvuvio huo, fomula ni hiyo hapo juu.. “tubu dhambi zako, kwa kumaanisha kuziacha kabisa, kisha katafute ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu sawasawa na Matendo 2:38, na Bwana ataleta uvuvio wa Roho Juu yako.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Roho Mtakatifu na Roho Takatifu?

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

6# SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Killian Baya
Killian Baya
1 year ago

Naomba nitumiwe mafundisho mbalimbali ya Bibilia