Adhama ni nini katika biblia?

by Admin | 29 March 2021 08:46 pm03

Adhama ni neno lenye maana ya “Uzuri wa hali ya juu sana”. Na huu uzuri ni Bwana Yesu tu peke yake ndio anao, yeye ndiye mwenye adhama.

Zaburi 93: 1 “Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele”

Mistari mingine michache inayozungumzia adhama ni kama ifuatayo..

Zaburi 96:6 “Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake”.

Zaburi 104:1 “ Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Wewe, Bwana, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama.

2 Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia;”

Isaya 33:21 “ Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo”.

2Wakorintho 4:7 “Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu”.

Mistari mingine iliyotaja neno hilo ni pamoja na 1Nyakati 16:27, Zaburi 21:5, Zaburi 113:3,  Zaburi 148:13 na Zaburi 29:4.

Hivyo Bwana Yesu, peke yake ndiye mwenye heshima yote na adhama yote, na wala hakuna mwingine.

Ufunuo 5:9 “Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa”

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).

Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)

UTUKUFU NA HESHIMA.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/03/29/adhama-ni-nini-katika-biblia/