Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

by Admin | 19 January 2022 08:46 pm01

Podo ni kimfuko au kibegi kidogo aidha cha ngozi au malighafi nyingine, ambacho hutumika kubebea mishale.

Utalisoma Neno hilo katika vifungu hivi;

Mwanzo 27:1-3
[1]Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
[2]Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
[3]Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;

Soma pia Ayubu 39:23, Isaya 49:2, Yeremia 5:16

Lakini Hiyo inafunua nini rohoni?
Sikuzote askari makini huwa habebi mchale mmoja anapokwenda vitani..atahitaji
Furushi la mishale kujihakikishia ushindi wake dhidi ya adui zake. Na ndio hapo atahitaji podo la kuihifadhia hiyo mishale yake.

Ni kama mwanajeshi, hawezi kutegemea risasi moja kujihakikishia ushindi atakuwa na mkanda wa risasi, ili adui yake ajapo amshindilie vya kutosha..

Halikadhalika na sisi kama wakristo, hatuna budi kuwa na podo zetu zenye mishale mingi ya kumpiga yule adui.
Hatumpigi shetani kwa maombi tu peke yake, vinginevyo tutakwama mahali.. tutampiga kwa mshale wa kuhibiri injili pia, kwa mshale wa kutenda matendo mema, kwa mshale wa kumtolea Mungu sadaka, kwa mshale wa kuwasaidia wenye uhitaji, kwa mshale wa utakatifu n.k.

Hapo ndipo tutakuwa tumezijaza podo zetu silaha.

Embu soma kwa makini vifungu hivi;

Zaburi 127:4-5
[4]Kama mishale mkononi mwa shujaa,
Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
[5]Heri mtu yule
Aliyelijaza podo lake hivyo.
Naam, hawataona aibu
Wanaposema na adui langoni.

Nasi tujitahidi kujaza podo zetu silaha nyingi ili shetani asipate upenyo wa kutushambulia kirahisi.

Bwana akubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?

Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).

KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/01/19/podo-ni-nini/