by Admin | 16 March 2022 08:46 am03
Tatizo la visigino kuuma ni ishara ya nini kibiblia?..Au visigino kuwaka moto?.
1) Visigino kuuma.
Kama unafanya shughuli yenye kuhusisha miguu, kwamfano kulima au kutembea umbali mrefu, au michezo..basi ni jambo la kawaida visigino kuuma, au visigino kuwaka moto.
Suluhisho la tatizo hilo ni kupunguza shughuli hizo zinazohusisha miguu, na miguu itarudia hali yake.
Lakini kama huna shughuli zozote unazozifanya na umeenda hospitali na hujapata suluhisho, na hujui sababu, na pengine umeshafanyiwa hata na maombezi, na tatizo bado lipo palepale..
Basi suluhisho la tatizo hilo,linaweza kuwa la kimaandiko,na maandiko yafuatayo yatakufungua…
Yeremia 13:22 “Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya WINGI WA UOVU WAKO, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia”.
Jiangalie maisha yako ni wapi hapako sawa na Mungu..tubu makosa yako kwa Mungu kwa kumaanisha kuyaacha.
Angalia mahali unapofanyia kazi, au mahali unapoishi, jinsi unavyoenenda, tafakari mawazo ya mioyo yako, je yanampendeza Mungu?..
Je unao upendo?, Wewe ni mvumilivu, ni mtu wa kusamehe au wa vinyongo?, Je ni mtu unayemcha Mungu na kumwogopa?.
Kama sio basi hiyo ndio sababu kwanini visigino vyako vinauma, au vinawaka moto, na umekosa ufumbuzi kila mahali.
Litafakari sana hilo na Mungu akusaidie, yeye ni mwaminifu tukiungama dhambi zetu kwa lengo la kuziacha kabisa, anatusamehe na kuponya magonjwa yetu na majeraha yetu, kwasababu lengo lake sio sisi tuteseke, bali tuwe na furaha na tupate mema, ndio maana saa nyingine anaruhusu vitu fulani vitutokee ili tutubu, na mwishoni atubariki zaidi.
Maran atha!.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/03/16/tatizo-la-visigino-kuuma-kibiblia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.