EE MUNGU, MUNGU WANGU, NITAKUTAFUTA MAPEMA:

EE MUNGU, MUNGU WANGU, NITAKUTAFUTA MAPEMA:

Daudi alikuwa ni kijana mdogo, lakini aliona jinsi muda unavyokimbia kweli kweli, aliona jinsi, siku zinavyotoweka kwa kasi, na huku bado hajatengeneza mambo yake sawa na Mungu.

Japokuwa katika hatua aliyofikia tayari alikuwa ni kipenzi cha Mungu, lakini hakuridhika na hali yake ya kiroho, akataka ayatengeneze mapema mambo yake na Mungu, asiwe na doa lolote kwake, Ndipo akaandika Zaburi hii akasema;

ZABURI 63:1 “Ee MUNGU, Mungu wangu, NITAKUTAFUTA MAPEMA, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji”.

Alijua thamani ya ujana wake, kwamba akiuacha tu ukiyeyuka, mpaka kufikia uzee bila kumtafuta muumba wake, atakuwa ameshindwa vita vikubwa vya Maisha.. Ndio maana akatia bidii sana, kumtafuta Muumba wake mapema, angali bado ni kijana mdogo. Akawa siriazi na Mungu wake,

Alilitambua vizuri lile andiko linalosema..

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.

Kwamba ipo miaka ambayo akiifikia mtu hatapata raha yoyote Maishani mwake, kama ujana wake uliishia katika mambo yasiyokuwa na maana.. Hivyo akasema, nitamtafuta Mungu wangu mapema, haijalishi ni mateso gani au vikwazo gani nitavipitia sasa, na akalithibitisha kweli lile alilolisema kwa vitendo.

Hakungojea uzee, au afikishe umri Fulani wa makamo ndio aache njia za uovu, hakufikia uzee ndio amfanye Bwana kuwa ngao yake.. Bali umri wake ule ule wa ujana alimtafuta Mungu wake kwa bidii.

Swali la kujiuliza na wewe kama kijana, au wewe kama mtu mzima, bado unaona una muda wa kusubiri kwa Mungu wako?

Mtafute Mungu wako mapema, kesho si yako. Hizo nguvu za kiroho Mungu alizoziweka ndani yako, hazitakuwepo kesho. Neema ya wokovu, huwa haidumu milele.
Inatabia ya kuzunguka na kuhamia kwa wengine, jambo ambalo watu wengi hawalijui. Ilikuwepo kwa wayahudi, lakini sasa ipo kwetu. Na Mungu ameahidi siku hizi za mwisho itaondoka kwetu itarudi kwa wayahudi tena. Je unalifahamu hilo?

Bwana Yesu alisema..

Yohana 11:9 “… Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.

Akimaanisha kuwa, nuru ya ulimwengu (yaani JUA) huwa linafanya kazi saa 12 tu. Baada ya hapo ni giza. Na ndivyo Yesu anavyoifananisha neema yake na JUA. Kwamba inadumu kwa kipindi Fulani tu, baada ya hapo haitaonekana tena.

Leo hii unaipuuzia injili, hutaki kutubu dhambi zako, kuna wakati nguvu ya kuvutwa kwa Yesu itaondoka kwako na kuamia kwa wengine. Kipindi hicho kikifika, milele hutakaa umgeukie Kristo utabakia kuwa mtu wa kudhihaki na kejeli kwenye mambo ya ki-Mungu. Kwasababu neema iliyokuwa inakuvuta imeshaondoka.

Kuwa makini sana na nyakati hizi za majeruhi. Mtafute Mungu wako mapema. Muda tuliobakiwa nao ni mchache mpaka Kristo atakapokuja, kizazi tunachoishi mimi na wewe, kimekidhi vigezo vyote vya kinabii kushuhudia tukio la unyakuo, na lile la kurudi kwa pili kwa Yesu duniani.. Unadhani tutakuwa na kizazi kingine? Soma biblia vizuri uone.

Unangoja nini?, Unamsubiria nani? Mgeukie Yesu mapema hii. Kanisa tulilopo ndio la saba na la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, (Ufunuo 3:14-21), Na hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili.

Tubu dhambi zako kwa kumaanisha,kweli kweli, mimina moyo wako kwa Bwana, salimisha ujana wako kwake, jitwike msalaba wako angali una kipindi kifupi bado, saa ya wokovu ni sasa, sio kesho, kama maandiko yasemavyo.

Ndugu, ikiwa unataka leo, kurudi kwa Bwana wako, na umedhamiria kwa dhati kufanya hivyo, basi fahamu Bwana Yesu anaweza kukupokea na kukusamehe dhambi zako.

Ni wewe tu kumaanisha kufungua moyo wako, kwani leo leo anaweza kukusamehe na kukupokea kama kiumbe kipya kwake. Akakusamehe kabisa dhambi zako. Basi Ikiwa upo tayari kufanya hivyo unaweza tafuta mahali pa utulivu, kisha piga goti, hata kwa machozi fuatisha sala hii ya toba kwa Imani, na Bwana atakusamehe;

Sema…

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.

Unaweza kirudia tena hiyo sala, hata mara mbili au tatu, mpaka utakaposikia amani moyoni mwako.

Basi ikiwa umekamilisha hilo..Hatua iliyobakia kwako ni ubatizo, kama hukubatizwa ipasavyo kwa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo.

Ikiwa utahitaji msaada huo na mafundisho ya kuukulia wokovu basi unaweza wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;

+255693036618/ +255789001312

Tafadhali shea na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?

WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.

HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments