Je Bwana Yesu aliruhusu wanafunzi wake kubeba Fimbo au hakuwaruhusu? (Marko 6:8 na Mathayo 10:10).

by Admin | 1 June 2023 08:46 am06

Swali: Tukisoma Marko 6:8, tunaona Bwana Yesu anawaruhusu wanafunzi wake “wabebe fimbo”, lakini tukirejea katika Mathayo 10:10 tunasoma habari tofauti, Bwana Yesu anawakataza wasibebe chochote hata fimbo..sasa mwandishi yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi? Je biblia inajichanganya yenyewe?.

Jibu: Biblia kamwe haijichanganya mahali popote, vinginevyo kitabu kizima kitakuwa ni cha uongo!. Lakini kama ni kitabu cha kweli kilichojaa maneno ya kweli ya uzima, na Roho Mtakatifu basi hakiwezi kuwa kitabu cha ushuhuda wa uongo!, au unaochanganya!..kinachochanganyikiwa ni fahamu zetu katika kukielewa kitabu hicho, lakini chenyewe kama chenyewe hakina kasoro yoyote.

Awali ya yote tuisome mistari hiyo…

Marko 6:7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;

8  akawakataza wasichukue kitu cha NJIANI ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;

9  lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili”.

Hapa ni kweli tunaona Bwana anawaambia wasibebe chochote ila Fimbo tu!… Tusome tena habari hiyo katika kitabu cha Mathayo..

Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

8  Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

9  Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;

10  wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, WALA FIMBO; maana mtenda kazi astahili posho lake”.

Hapa tunaona Bwana anawakataza hata Fimbo wasibebe, na ilihali kule kwenye kitabu cha Marko tunaona anawaambia wasibebe kitu kingine chochote isipokuwa Fimbo tu!.. Sasa mwandishi yupi ni wa kweli na yupi ni wa uongo?.

Jibu ni kwamba waandishi wote ni wa kweli hakuna aliye mwongo!,

Katika Marko Bwana anawaambia wasibebe vitu vya njiani isipikuwa FIMBO TU!.. Sasa fimbo hakikuwa chakula bali ni kifaa kinachomwezesha mtu kutembea katika milima na mabonde! Ni kama tu kiatu kilivyo msaada kwa miguu katika safari ndefu za miiba na mavumbi.. Fimbo na yenyewe ilikuwa ni hivyo hivyo..

Kwahiyo fimbo ilikuwa ni sehemu ya kitu cha msingi mtu anachoweza kuwa nacho kwa safari kama tu vile mtu alivyo na kanzu au kiatu au nguo.

Lakini sasa Bwana alichowakataza ni wao kubeba fimbo ya pili au ya tatu, kana Kamba moja ikivunjika basi kutakuwepo na akiba. Hicho ndicho kitu Bwana alichowakataza akawaambia wabebe fimbo moja tu!. Wasihofie endapo hiyo waliyonayo itapata itilafu, kwani huko wanakokwenda Mungu wa mbinguni atawafungulia mlango watapata nyingine.

Lakini pia sio Fimbo tu!, bali hata kanzu!.. wasibebe na kujifungasha mizigo ya kanzu nyingi, waende na hiyo moja tu iliyopo mwilini kwasababu huko waendako Baba yao wa mbinguni anajua kuwa wana haja na nazo, hivyo wasitie wasiwasi kwasababu mtenda kazi amestahili posho yake (watapata huko waendako). Ndio maana akawakataza wasibebe kanzu mbili…

Marko 6:8 “akawakataza wasichukue kitu cha NJIANI ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;

9  lakini wajifungie viatu; akasema, MSIVAE KANZU MBILI”.

Hapo mwisho anasema “msivae kanzu mbili” maana yake ile moja waliyonayo mwilini inatosha.. vile vile wasibebe fimbo nyingine ya pili, hiyo moja watakayokuwa nayo inatosha!..sawasawa na hiyo Mathayo 10:10..

Kwahiyo biblia haijichanganyi, bali shetani ndiye anayetuchanganya….

Sasa kufahamu ni somo gani tunaloweza kujifunza nyuma ya hii habari fungua hapa>>> Bwana alimaanisha nini kusema“maana mtenda kazi astahili posho lake”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Je suruali ni vazi la kiume tu?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).

Je! habari ya muda aliotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/06/01/je-bwana-yesu-aliruhusu-wanafunzi-wake-kubeba-fimbo-au-hakuwaruhusu-marko-68-na-mathayo-1010/