Bwana alimaanisha nini kusema“maana mtenda kazi astahili posho lake”

Bwana alimaanisha nini kusema“maana mtenda kazi astahili posho lake”

Moja ya maagizo ambayo Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake alipowatuma kwenda kuhubiri injili mbali, lilikuwa ni kutokulipisha fedha katika huduma yoyote watakayoitoa, halikadhalika   kutokubeba chochote katika safari yao. Yaani wasiwe na maandalizi yoyote ya njiani, Lakini mwishoni kabisa mwa maagizo yake aliyasema maneno haya “maana mtenda kazi astahili posho lake”.. Sasa swali linakuja Je hili posho ni lipi alilostahili huyu mtandakazi ili hali ameitwa atoe bure?

Mathayo 10:8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;

10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake”.

JIBU: Posho alilostahili ni lile ambalo Bwana Yesu mwenyewe atampa katika kazi ya injili anayoipeleka, kwa kupitia watu wakarimu ambao Bwana Yesu mwenyewe atawagusa moyo huko waendako aidha kwa kuwapa maji, au chakula, au nguo, na wakati mwingine hata fedha.

Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Bwana Yesu anaweza kumtunza mtumwa wake, katika mazingira yoyote atakayomtuma. Na ndio maana mwishoni kabisa akawaambia maneno haya;

Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!

Ni ni kufunua kuwa hatupaswi kuwa na wasiwasi wa maandilizi yoyote ya huduma ya Kristo, pale ambapo hatuna chochote,  Bwana anataka tuwe wepesi (SIMPLE), tusijali sana tutakula nini, tutavaa nini huko tuendako, kesho tutatolea wapi nauli ya kurudi, hilo jambo Bwana hataki sisi kama watumwa wake tulifikirie, kwasababu ameahidi kabisa ikiwa tunatenda kazi yake kiuaminifu, basi tumestahili posho lake, hivyo anza kutumika.

Lakini haimaanishi kuwa, wakati wote, hata kama unacho, ndio ujifanye hauna, hapana, bali, upo wakati wewe kama mtumishi wa Mungu utabarikiwa na utakuwa na vya kuendea huko katika ziara, hivyo vitumie hivyo, Na ndio maana wakati mwingine Bwana aliwaambia wajibebe fimbo ya njiani, na kujifungia viatu, wakati sehemu nyingine kama tuliyosoma hapo juu aliwakataza.(Marko 6:8-9)

Kwahiyo, kwa vyovyote vile, Bwana atatunza, ilimradi tunamtumkia yeye kwa uaminifu. Tusiwe na wasiwasi na huduma yake, Haleluya..

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

ANGALIENI MWITO WENU.

WITO WA MUNGU HAUVUKI NENO LAKE.

MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
9 months ago

Asante Mungu akubariki sana mtu ishi

M
M
1 year ago

Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
1 year ago

Asante sana mwalimu kwa mafundisho mazuri na barikiwa sana pia.Binafsi nimekuelewa vizuri.Lakini pia nina swali.Je,vigezo vya kwenda kuwahubiria wengine habari za wokovu ni vipi?Je,aweza mtu kuwahubiria wengine habari za wokovu hali yeye mwenyewe HANAO huo wokovu? Asante!