Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Jibu: Biblia haijichanganyi mahali popote na haijawahi kujichanganya isipokuwa viwango vyetu vya kutafakari ndivyo vinavyotufanya  tuone kuna utata mwingi kwenye biblia (na kumbuka tunapozungumzia biblia tunamaanisha ile yenye vitabu 66) na si zaidi ya hivyo!.

Vitabu 66 vya biblia ndivyo vilivyohakikiwa na Roho Mtakatifu kwa vizazi vyote kama Neno la Mungu lililo hai.

Sasa kabla ya kwenda kuitafakari mistari hiyo hebu tuisome kwanza..

Mwanzo 15:13 “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa MIAKA MIA NNE

14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi”

Tusome tena,..

Kutoka 12:40 “Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa NI MIAKA MIA NNE NA THELATHINI. 

41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo MIA NNE NA THELATHINI, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri”.

Sasa swali ni hili, Mungu alimdanganya Abramu kuwa uzao wake utakaa miaka 400 na kumbe ni miaka 430?, je Mungu ni mwongo?

Jibu ni la! Hakudanganywa, kwasababu hiyo miaka 430 bado ipo katika namba mia nne, Mungu hakumwambia kuwa atakaa miaka mia nne kamili, bali alimwambia tu miaka mia nne, ikiwa na maana kuwa inaweza kuwa ni miaka mia nne kamili au miaka 410 au 430 au 470 au hata 490 lakini haitazidi hiyo miaka 400 na kuwa 500.

Ni sawa mtu na mtu akuulize wewe una miaka mingapi na umwambie una miaka 30 au 40, unaweza kumpa namba ya ujumla lakini kiuhalisia huenda unayo miaka 30 na miezi 6 au na miezi 7,au una miaka 40 na miezi 8 au 9.. Kwahiyo wewe kumwambia kuwa una miaka 30 au 40 unakuwa hujamdanganya.. Ni kweli ndio miaka yako, isipokuwa hujapenda kumwambia na miezi iliyo mbele ya hiyo miaka..Ungekuwa umemdaganya endapo kama ungemwambia unayo miaka 30 kamili au 40 kamili, hapo utakuwa umemdanganya!..

Vile vile Bwana Mungu hakumwambia Abramu kuwa Uzao wake utakaa utumwani miaka 400 kamili, bali alimwambia tu utakaa miaka 400.. Na ndivyo ilivyokuwa.

Kwahiyo biblia haijichanganyi.. Tazama pia miezi aliyotawala Yekonia je unajichanganya? >>> YEKONIA ALITAWALA MUDA GANI?

Je umeokoka?..kumbuka kuwa hizi ni siku za mwisho, na unyakuo wa kanisa ni muda wowote kuanzia sasa.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! kuna mambo ambayo Mungu hawezi kuyafanya kulingana na Waamuzi 1:19?

Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?

Je! habari ya muda aliyotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).

Je! biblia inajichanganya katika 1Petro 2:13 na Matendo 5:29.

Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
filomena mulembule
filomena mulembule
9 months ago

Amen nimeelewa

Anonymous
Anonymous
9 months ago

Je,Bibilia inaposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu inamaanisha nini?