Je! habari ya muda aliotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).

Je! habari ya muda aliotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).

Jibu: Kabla ya ufafanuzi tuisome mistari hiyo..

2Wafalme 24:8 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala MIEZI MITATU katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani wa Yerusalemu”.

Tusome tena,

2Nyakati 36:9 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu MIEZI MITATU NA SIKU KUMI; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana”.

Hapa tunaona mwandishi wa kitabu cha Wafalme anataja miezi aliyotawala Yekonia ni mitatu (3) lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati ameongeza siku kadhaa mbele yake (miezi 3 na siku 10).

Swali, je! Ni yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.. au je biblia inajichanganya?. Au ina makosa katika uandishi?

Jibu ni la! Biblia haijichanganyi mahali popote na haijawahi kujichanganya, na wala haina makosa mahali popote kwasababu endapo ikijichanganya au ikikosewa, basi yote itakuwa ni uongo na sio Neno la Mungu, lakini tunaona maneno yaliyoandikwa kule ni nguvu ya Mungu, na ni uweza wa Mungu, na tena ni Roho, na hayana makosa…

Sasa tukirudi katika hiyo habari ya muda aliotawala Yekonia, je! Mwandishi yupi yupo sahihi?.

Jibu ni kwamba wote wapo sahihi, hakuna aliyekosea.

Mtu akikwambia nitakuja kukutembelea mwezi wa 3 halafu akaja mwezi huo wa 3 tarehe 10 je atakuwa amekudanganya?..bila shaka atakuwa hajakudanganya kwasababu hiyo tarehe ipo ndani ya huo mwezi wa tatu (haijatoka ndani ya huo mwezi wa 3).. hata kama atakuja tarehe 20 au 21 au 25 atakuwa bado hajakudanganya kwasababu bado tarehe hizo zipo ndani ya mwezi wa huo wa tatu.

Hali kadhalika Mwandishi wa kitabu cha Samweli kasema tu “Yekonia katawala miezi 3” ingawa alikuwa anajua na siku alizotawala lakini kapenda tu kufupisha, hajapenda kutaja na siku wala masaa wala dakika wala sekunde lakini kafupisha tu! Miezi 3.

Lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati kapenda kutaja Miezi Mfalme Yekonia aliyotawala na Siku alizotawala, lakini hajapenda kutaja na masaa wala dakika wala sekunde… Huwenda angetokea na mwandishi mwingine angetaja Miezi aliyotawala, na siku na masaa na sekunde!.. na bado asingekuwa ametoa taarifa sahihi ambazo hazikinzani na za wale waliofupisha!.

Kwahiyo biblia haijajichanganya hapo!.wala haijichanganyi mahali popote. Tazama pia muda wana wa Israeli waliokaa Misri je ni miaka 400 au 430?..kujua hilo kwa urefu fungua hapa >>> Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Je unajua kuwa dhiki kuu itakuja baada ya unyakuo wa kanisa na unyakuo upo karibu?..tutumie ujumbe inbox kwa maelezo marefu juu ya hili.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

MIEZI 13 YA KIYAHUDI.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

TUSIIFUATISHE KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU.

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kambale Kihumbira
Kambale Kihumbira
1 year ago

MUNGU awabariki kwa kutubariki