Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani.

by Admin | 22 October 2024 08:46 pm10

Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani?

Kitabu cha Waebrania ni moja ya nyaraka ambazo waandishi wake hawajajitambulisha aidha ndani au mwanzoni  au mwishoni mwa nyaraka hizo. Lakini kwa kutathimini baadhi ya nukuu za mwandishi, huwenda alikuwa ni mtume Paulo aliyeuandika. Kufuata na kumtaja Timotheo kwenye waraka huo, na tunajua Timotheo alikuwa chini ya utume wa Paulo, kwani  ndiye aliyeongozana naye na kumtaja sana katika nyaraka zake nyingi.

Waebrania 13:23  Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.

Na pia jinsi mwandishi alivyomalizia waraka wake,  kwa kusema “neema na iwe nanyi nyote”.  Ni salamu inafanana na nyaraka zote za mtume Paulo, kila alipomaliza alihitimisha na  baraka hizo.

Japo wengine wanasema namna ya uandishi haifanani na mtume Paulo, yawezekana alikuwa ni Apolo, au Barnaba, au sila au mtu mwingine tofauti na Paulo.

Lakini kwa vyovyote vile kumtambua mwandishi, si lengo la uandishi, lengo ni kufahamu kilichoandikwa ndani humo.

Maelezo mafupi ya kitabu hichi.

Kwa ufupi, kama kitabu hichi kinavyoanza kujitambulisha,  kinasema

WARAKA KWA WAEBRANIA.

Maana yake ni kitabu kilichoelekezwa kwa wayahudi-wakristo waliokuwa katika kanisa wakati ule. Ndio maana kwa jinsi ulivyoandikwa waraka huu, mwandishi anazungumza na mtu ambaye mwenye uelewa wa dini ya kiyahudi na taratibu zake za kiibada.

Dhumuni kuu ni kueleza UKUU WA YESU JUU YA WATU WOTE, NA MAMBO YOTE YA AGANO LA KALE.

Kwamfano anaeleza Yesu alikuwa mkuu juu ya;

  1. Manabii wa agano la kale

Waebrania 1:1  Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2  mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3  Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu

  1. Alikuwa mkuu zaidi ya malaika: Soma Waebrania 1:13-2:18

Waebrania 1:13  Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14  Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

  1. Alikuwa mkuu zaidi ya Musa, Yoshua na Haruni. (Soma, Waebrania 3:1-19, 4:1-13, 4:14-10:18)
  2. Alikuwa mkuu zaidi ya kafara za agano la kale. (Soma, Waebrania 10:11-14).

Waebrania 10:11  Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.

12  Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

13  tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14  Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.

Hivyo kitabu hichi kinamfafanua Kristo kwa undani, jinsi alivyo na ukuu zaidi ya mambo yote ya agano la kale. Na kwamba watu wote tangu Adamu mpaka Ibrahimu wasingeweza kukamilishwa bila Kristo. Waliishi wa ahadi hiyo ya kuja mkombozi, wakiingojea kwa shauku na hamu (Waebrania 11).

Lakini pia kitabu hichi  kinatoa angalizo kwa wayahudi wasirudi nyuma kwasababu ya dhiki na mateso yanayowapata kwa ajili ya imani ya Yesu Kristo. (Waebrania 12:1-13, 10:26-31), Bali wamtazame Kristo kama kielelezo chao, jinsi alivyostahimili mashutumu makuu namna ile.  Hii ni kutuhamasisha na sisi kuwa tunapopitia dhiki leo basi nasi tumtazame Kristo aliyestahili, mapingamizi yale, wala hakuutupa ujasiri wake.

Waebrania 12:1  Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2  tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume.

Ielewe kwa kina Waebrania 13:5 maana yake.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Je ni Mungu au Malaika?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/10/22/mwandishi-wa-kitabu-cha-waebrania-ni-nani/