Ipi tofauti kati ya sherehe, Sikukuu na karamu kibiblia?.

Ipi tofauti kati ya sherehe, Sikukuu na karamu kibiblia?.

Jibu: Tutazame moja baada ya nyingine.

     1. SHEREHE.

Katika Biblia hamna neno “sherehe” lakini kuna neno “sikukuu”.

Sherehe ni shughuli (tukio) la kijamii linayofanyika kwa lengo la kuadhimisha, kukumbuka jambo fulani  (kama vile  harusi, mahafali, siku ya kuzaliwa, ushindi n.k),

Na sherehe huwa inaambatana na michezo, au hotuba,  au ibada au michezo, kutegemea na aina ya sherehe..(na katika Biblia hatuna neno sherehe).

Kama jina sherehe lilivyo maana yake linahusisha “shangwe” au “shamra shamra”.

   2. SIKUKUU.

Sikuukuu ni neno linalopatikana kwenye Biblia, na tafsiri ya Neno Sikukuu ni “Siku iliyo kuu”. (Yaani siku yenye ubora kuliko nyingine)

Na katika Biblia zinatajwa sikukuu kadha wa kadha, ambazo hazikuwa kwa lengo la ibada na tafakari za kiMUNGU, mfano wa sikukuu hizo ni sikukuu ya vibanda, pasaka, na baragumu.

Kwa urefu juu ya Sikukuu hizo na maana zake kiroho fungua link ifuatavyo.

https://wingulamashahidi.org/archives/1858Karamu.

   3. KARAMU.

Karamu ni neno linalopatikana kwenye Biblia ambalo lina maana ya tafrija yenye mandalizi ya chakula.

Kwa ufupi ni shughuli yoyote ndogo au kubwa yenye malengo makuu ya kula vyakula na kufurahi kutokana na tukio fulani jema.

Katika Biblia kunatajwa karamu mbalimbali mfano wa hizo ni ile Abramu aliyowafanyia wale Malaika wawili waliomtembelea.

Mwanzo 19:1 “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.

2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.

3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. AKAWAFANYIA KARAMU, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.”

Na ile Abramu aliyomfanyia mwanae baada ya kuachishwa maziwa.

Mwanzo 21:8 “Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.”

Lakini ipo karamu iliyo kuu katika Biblia ambayo haipaswi mtu yoyote kuikosa ambayo ni ile ya Mwanakondoo.

Kwa urefu juu ya karamu ya mwanakondoo ni fungua link ifuatayo..

https://wingulamashahidi.org/archives/1280

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply