Jibu: Kwa asili Kuomba sio karama bali ni “Agizo”.
Na agizo la kuomba si la mtu mmoja bali ni la watu wote wenye karama zote,
Kwasababu hata mwenye karama ya kinabii ni lazima awe mwombaji kwa lengo la kuinoa karama yake au kuwaombea wale aliowapa unabii..
Vile vile mwenye karama ya uponyaji ni lazima aombe na kufanya maombezi ili mgonjwa/wagonjwa wapone.
Mwenye karama za lugha ni ivyo hivyo ni lazima aombe ili anene kwa lugha, matendo ya miujiza ni ivyo hivyo ni lazima maombi yahusike ili miujiza itendeke.
Nabii Eliya hakushusha moto kutoka mbinguni kwa uweza wa MUNGU bila kuhusisha maombi, aliomba kwanza ndipo muujiza ukatendeka..na karama zote zinaendeshwa na maombi.
Sasa tunarudi kwenye swali, je kuna karama ya kuomba na maombezi?.
Jibu ni La! Hakuna hiyo karama, kwasababu agizo haliwezi kuwa karama..
Lakini sasa kama ni hivyo inakuwaje wapo watu wenye uwezo wa kuomba kwa kina na masafa marefu kuliko wengine?.
Kuna sababu kuu mbili (02) za hali hiyo ya baadhi ya watu kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya wengine, na sababu ya pili ina uzito zaidi kwa mujibu wa swali Letu.
1. MAZOEZI YA UTAUWA.
Najua unajiuliza mazoezi ya Utauwa ni kitu gani?…tusome maandiko yafuatayo kisha tufafanue.
1 Timotheo 4:7 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; NAWE UJIZOEZE KUPATA UTAUWA. 8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”
1 Timotheo 4:7 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; NAWE UJIZOEZE KUPATA UTAUWA.
8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”
Kiswahili kingine cha mazoezi ya utauwa ni “mazoezi ya uungu”.. yaani mtu anakuwa na mazoezi ya kutosha ya maagizo ya MUNGU kama maombi, mifungo, na uinjilisti…kiasi kwamba anakuwa ni mtu anayejizoeza kuhubiri mara kwa mara, au kuomba mara kwa mara jambo linalofanya uwezo wake wa kuomba, kuhubiri au kufunga kuongezeka kila iitwapo leo.
Sasa kundi hili linalojizoeza utauwa huwezi kushindana nalo wewe unayejizoeza kulala kutwa kuchwa au kula mara tatu kwa siku.
Wewe utasali dakika mbili na kulala mwenzio atasali masaa 5 bila kuchoka, wewe utabaki kusema fulani ana karama ya kuomba kumbe ni uvivu wako tu uliovikwa na ibilisi.
Hiyo ni sababu ya kwanza…
2. KARAMA YA MASAIDIANO.
Hii ndio karama inayochanganywa na wengi..
1 Wakorintho 12:28 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha”.
Katika karama hii ya masaidiano ndio hapa kuna watu wanakuwa na mzigo wa kuomba kwaajili ya wengine kwa muda mrefu kwasababu ndani yao kuna msukumo wa kusaidia.
Ile roho ya kutamani kusaidia inamfanya mtu aidha atoe vitu vyake au muda wake katika maombi na kuomba mpaka ule mzigo utakapoisha ndani.
Kwahiyo kwa hitimisho hamna karama ya maombi kwenye Biblia, bali ya masaidiano ambayo inahusisha maombi au kitu kingine chochote cha kumsaidia mtu mwenye uhitaji.
Je wewe ni mwombaji?. Kama sio. fahamu shetani kafaulu pakubwa sana kukupata, kuelewa faida za maombi kwa undani wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo, tutakupa masomo husika bure.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ