Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi.
Utangulizi: Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno la kusimama nalo ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu na tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kwa kusimama na maandiko ya Biblia.
Biblia inataja ulimi wa mtu, kama kiungo kiharibifu kuliko viungo vyote katika mwili.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
Sasa kwasababu ulimi ni kiungo hatarishi,maana yake kinaweza kumfanya mtu kuanguka moja kwa moja pasipo kuamka tena, hivyo andiko hili halijahifadhiwa ndai ya Biblia liwe tangazo la taarifa tu, kwamba tujue hatari ya ulimi halafu basi.
Hapana, si lengo la maandiko yote ya Biblia, bali maandiko yote yana lengo la sisi kusoma, na kujitengeneza kulingana na andiko hilo kwa njia ya kuomba…hivyo tumia muda kuomba maombi yafuatayo
1. OMBA UTAKASO WA ULIMI.(tumia Dk. 30 au zaidi).
– Takasa kinywa chako, kwa kutubia maneno yote mabaya na mazungumzo yasiyofaa yaliyotoka kinywani mwako na omba utakaso kwa damu ya YESU.
2. MWOMBE BWANA AKAKUTENGENEZE MANENO YA KINYWA CHAKO.
– Ukanene kwa hekima.
Zaburi 49:3 “Kinywa changu kitanena hekima,
Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara”
Ukanene kweli siku zote usiseme uongo.
Mithali 8:7 “Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu”.
3. OMBA ULINZI WA KINYWA.
Mithali 13:3 “Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu”.
– Usiwe mtu wa kupayuka.
Zaburi 141:3 “Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu”
– Usifanye dhambi (mf. Uongo, usengenyaji, matukanio, malalamiko na faraka).
Ayubu 31:30 “(Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
4. KEMEA KILA ROHO INAYOJIINUA KUKUKOSESHA KUPITIA ULIMI (KINYWA) CHAKO.
Kemea kwa jina la YESU KRISTO kila pando la la uongo, usengenyaji ndani yako, kanisani kwako, familia yako na wakristo wenzako wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ