Desturi ya maziko kibiblia ilikuwaje?.

Desturi ya maziko kibiblia ilikuwaje?.

Swali: Je Desturi ya kuzika ilikuwaje, ikiwemo upakaji wa manukato maiti?


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa katika Biblia, hakukuwa na sheria ya kuvika sanda mwili wa mtu aliyekufa, wala kuupaka manukato,

Mtu akifa anakuwa amekufa, na liliobaki ni moja tu kwake, kwamba mwili wake uzikwe.

Desturi ya kuvika mwili wa marehemu sanda na kuupaka manukato ulikuja baada ya wana wa Israeli kurudi kutoka Babeli, ambapo marabi wa kiyahudi waliaanza kuutumia huo utaratibu wa kuuvika mwili wa marehemu kitambaa cheupe na kuupaka manukato.

Na pia katika nyakati za Biblia, watu hawakuzikwa kwenye majeneza ya mbao kama ilivyozoeleka leo, badala yake walizikwa kwenye mapango ya asili au makaburi yaliyochongwa kwenye miamba (kama lilivyokuwa kaburi la Abrahamu huko Makpela, Mwanzo 23:19 au kaburi la BWANA wetu YESU KRISTO)

Baada ya miaka kadhaa, miili ikishaoza na kubaki mifupa tu, mifupa hiyo ilikusanywa na kuwekwa kwenye sanduku dogo la mawe  au kuwekwa sehemu moja na mifupa ya mababu zao (ndio maana ya msemo wa kibiblia “alilazwa pamoja na mababu zake”).

Mwanzo 49:33 “Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake”.

Na katika Biblia pia hakukuwa na sheria ya kuchoma maiti bali miili yote ilizikwa kwa heshima.

Sasa swali?.. Ni kwanini akina Maramu Magdalena na wale wanawake wengine walikwenda kaburini mapema siku ya kwanza ya juma kumpaka Bwana Manukato?.

Marko 16:1 “Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;

3 wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?”

Kulingana na mapokeo hayo ya wayahudi ambayo yalianza baada ya wao kutoka Babeli (lakini si agizo la Musa), ilikuwa ni sharti mwili uandaliwe kwa kupakwa manukato kabla ya kuzikwa.

Lengo la kufanya hivyo ni kupunguza harufu kipindi mwili unaanza kuoza, na kwasababu hawakuzika ardhini kama inavyofanyika sasa hivyo kama mwili usipopakwa hayo manukato harufu ingewasumbia wapita njia nje na mapango hayo, hivyo kulizuia hilo na kutunza heshima ya marehemu waliipaka miili manukato.

Na pia miili ya wanaume iliandaliwa na wanaume na wanawake iliandaliwa na wanawake, lakini katika mazingira fulani maalumu iliruhisiwa miili ya wanaume kuandaliwa na wanawake wa karibu sana, hususani wale wana familia wa karibu kutunza heshima na faragha ya marehemu., lakini haikuruhusiwa wanaume kuiandaa mikli ya wanawake kwa mazingira yoyote yale.

Sasa swali lingine kwanini akina Mariamu waende siku ya 3 na si ile siku aljyokufa?.

Jibu ni kuwa Kristo alikufa ijumaa jioni, hivyo nafasi ya kuuandaa mwili ilikuwa ni ndogo sabato ilikuwa imekaribia, na haikiruhisiwa kufanya maziko siku ya sabato.

Hivyo akina Yusufu na Nikodemo, waliuandaa ule mwili kwa hafaka haraka na kuufungua manukato, na wanawake walktama kuundaa vizur zaidi na kwa utaratibu.

Swali je na sisi ni kosa kuzika watu kwenye majeneza au ardhini? Au kutoipaka miili manukato? Au je ni lazima kuuvisha mwili sanda?.

Jibu ni la! Si kosa kuzika mtu kwenye jeneza  na pia si lazima kuvika maiti sanda kwani hata desturi hiyo haikutoka kwa MUNGU, asili yake ni wapagani ambapo ili kuweka usawa wa matajiri na masikini, wote walifungwa kwenye kitambaa cheupe, kwani hapo kwanza matajiri walizikwa na nguo za thamani na masikini kwa nguo za hadhi ya chini.

Kwahiyo si desturi ya lazima, na pia si kosa kuzika mwili kwa sanda kama Bwana YESU alivyozikiwa.

Lililo kubwa na la kuangalia sana ni wapo roho zetu zinapokwenda baada ya kufa, je tutaurithi uzima wa milele au tutapotea kwenye moto wa milele.

Lakini kufikiri juu ya maiti na mavazi yake, kwamba tutazikwaje ni tafakari dhaifu zisizotusaidia.

Je umeokoka?..una uhakika Bwana YESU akija leo unaenda naye?.

Kama hauna uhakika huo una subiri nini?. Mpe YESU maisha yako aiku ya leo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply