by Admin | 7 March 2020 08:46 pm03
SWALI: Mimi Nina MUNGU Wangu ambae Ni ALLAH subhanallah…sasa kwanini nimkabidhi maisha Yesu wakati naye alizaliwa Kama mimi?
JIBU: Mama yako alizaliwa kama wewe…lakini ilifika wakati Mwenyezi Mungu aliyakabidhisha maisha yako kwake. Ili uwe salama, ulindwe, uhifadhiwe, ulishwe na upendwe..na pamoja na hayo ufundishwe kanuni za maisha ambazo peke yako bila wazazi au mlezi usingeweza kujifunza.
Vivyo hivyo ulipaswa ukae chini ya sheria za wazazi wako ndipo uweze kufanikiwa, endapo ungekuika sheria hizo basi maishani usingefanikiwa….Na kama sio Mwenyezi Mungu kuyakabidhisha maisha yako kwa wazazi wako ambao wamezaliwa kama wewe, maisha yako yangukuwa magumu sana hapa duniani au hata pengine usingezaliwa kabisa au kama ungezaliwa ungekufa.
Vivyo hivyo Yesu alizaliwa kama sisi tulivyozaliwa, (Ingawa hakuzaliwa na dhambi ya asili kama sisi, kwasababu mimba yake ilitungishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu), na katika nyakati hizi za uovu na mateso na dhiki za ulimwengu.
Mungu kwa huruma zake na kwa jinsi anavyotupenda akamtuma huyu Yesu Kristo, ili awe kama mzazi kwetu kwasababu sisi wenyewe hatutaweza kwa nguvu zetu na kwa akili zetu kujiongoza..Ndio maana hatuna budi wote tuyakabidhi maisha yetu kwake ili tuwe salama sasa na ahera.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”
Yesu anapoingia maishani mwetu, anatupa furaha, faraja, amani, upendo na tunapata ulinzi dhidi ya Adui shetani na mapepo yake yote, siku zote za maisha yetu na tumaini la uzima wa milele.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/03/07/kuna-haja-gani-ya-kumwamini-yesu-aliyezaliwa-kama-sisi/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.