Wafilisti ni watu gani.

by Admin | 11 July 2020 08:46 pm07

Wafilisti ni watu gani?


Wafilisti ni watu walioishi kaanani ambao waliokuwa maadui wakubwa sana wa Israeli enzi za agano la Kale. Hawa walikuwa ni kundi mojawapo la wenyewe wa nchi ile  kabla ya Israeli kuifikia kutoka Misri.

Lakini wana wa Israeli walipokiuka maagizo ya Mungu ya kuwaua wenyeji wote wa miji ile yaliyoikuta,ili wamiliki, wao wakazembea hawakuwaua wote, kinyume chake wakawabakisha baadhi yao ikiwemo hawa wafilisti na ndio hao baadaye wakaja kuwa mwiba mkubwa sana kwao kama vile Mungu alivyowaambia.

Kipindi baada ya kipindi walikuwa wakiwashambulia waisraeli, na walipomlilia Mungu, (Waamuzi 10:7-8 ), basi Mungu aliwanyanyulia waamuzi wa kuwaokoa kutoka katika mateso yao, mfano Samsoni.

Wafilisti kwasasa ndio Wapalestina, unaowasikia pale mashariki ya kati, jina hilo lilizaliwa kutoka katika lugha ya wagiriki, ambao waliwaita wafilisti wapalestina. Na ndio mpaka sasa limezoeleka hivyo.

Wafilisti ni nchi gani?

Kama tulivyoona wafilisti ni watu waliokutwa kaanani kabla ya wana wa Israeli, lakini sio taifa au nchi. Japokuwa enzi zile walikuwa na miji yao mikuu mitano nayo ni.

  1. Gaza,
  2. Ashdodi,
  3. gathi,
  4. Ashkeloni, na
  5. Ekroni 

(1Samweli 6:17, Yoshua 13:3).

Walikuwa na wakuu/Wafalme wao watano pia kila mmoja na mji wake soma (Waamuzi 3:3). Sasa Miji hii yote ilikuwa kusini magharibi mwa taifa la Israeli.

Lakini Habari za wafilisti zinatufundisha nini?

Yapo mambo ambayo Mungu anaweza kutuagiza kufanya yakayazembea na madhara yake yakawa  mpaka vizazi vya baadaye, kama vile tunavyoona hawa wafilisti/Wapalestina, hawakuwa mwiba tu kwa Israeli wakati ule..Bali hata sasa ni mwiba mkali sana..Kama wewe ni mfuatiliaji wa diplomasia za kimataifa utaweza kufahamu ni kitu gani kinaendelea pale Israeli saa hii , kila kukicha ni machafuko.

Hivyo tuwe makini sana na maagizo ya Mungu, anayotuagiza tusiyapuze hata kidogo,..

Na agizo mojawapo ni wokovu. Jiulize je umelizingatia?.Kumbuka biblia inasema, Yesu ndiye njia, kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye.. (Yohana 14:6)..Hivyo kama bado hujaokoka, basi ndugu fanya hivyo mapema, ili njia ya mbinguni uione angali nafasi unayo.

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Na wakati wowote Yesu anarudi kulinyakua kanisa lake, dalili zote zinaonyesha kuwa mimi na wewe tupo katika majira hayo ya kurudi kwa Kristo mara ya pili, kutokana na hali halisi inayoendelea sasa hivi duniani. Hakuna asiyejua kuwa tunaishi katika majira hayo

Hivyo tatufa wokovu kwa bidii, kama haukuwa nao.

Bwana akubariki.

Tafadhali angalia pia na mada nyingine chini..usipitwe.

Mada Nyinginezo:

MALAKI, NABII WA MWISHO KATIKA ISRAELI.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MAONO YA NABII AMOSI.

HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

MATENDO YETU YANAPIMWA KATIKA MIZANI.

MPINGA-KRISTO

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/11/wafilisti-ni-watu-gani/