Kuota unachimba viazi, mihogo,madini n.k Kuna maanisha nini?

by Admin | 4 October 2020 08:46 pm10

Kuota unachimba viazi, mihogo, vitunguu, karoti, madini n.k Kuna maanisha nini?


Inategemea na maisha unayopitia sasa, ikiwa shughuli zao za mara kwa mara ni za migodini au mashambani hususani katika kazi hizo za kulima viazi, au vyakula vya ardhini, basi ndoto kama hizo kujirudia rudia  ulalapo litakuwa ni jambo la kawaida sana kwasababu biblia inasema ndoto huja kutokana na shughuli nyingi Mhubiri 5:3,

Hivyo kama upo katika mazingira hayo, basi ndoto hiyo usiitilie maanani sana kwasababu haibebi ujumbe wowote wa rohoni, zaidi sana hizo ni ndoto za mwili.

lakini ikiwa sivyo na imekujia kwa namna ya kipekee, yaani kwa uzito Fulani, basi inaweza ikawa ishara ya kuwa Mungu anakufungulia milango ya rizki mbeleni.

Biblia inasema.

Ayubu 28:5 “Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; …”.

Unaona, hivyo ikiwa utakaa katika hali ya kuyatenda mapenzi ya Mungu, basi ipo milango mingi sana, Mungu kakuwekea mbele yako, kwa hicho unachokifanya, na hata zaidi ya hapo. Ni wewe tu kuishi maisha yampendezayo Mungu wako.

Kwa muda wako soma, Kumbukumbuku la Torati sura ya 28 yote uone Baraka Mungu alizowawekea wale wote watakaoyashika maagizo yake kwa bidii.

Hivyo ili na wewe ndoto hizo ziwe kweli, hakikisha kwanza Kristo yupo ndani yako, kama hujaokoka hakikisha una mkabidhi Kristo maisha yako leo, na pia kuanzia huu wakati unaishi maisha kulingana na yeye anachotaka kulingana na Neno lake, baada ya hapo kuwa tayari kwa wema wake kujidhihirisha maishani mwako, lakini nje ya hapo, hilo linaweza lisikufikie kabisa.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Au jiunge moja kwa moja whatsapp kwa kubofya chini.

Group la whatsapp  Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

KUOTA UNAJIFUNGUA.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/10/04/kuota-unachimba-viazi-mihogomadini-n-k-kuna-maanisha-nini/