by Admin | 17 October 2020 08:46 pm10
Kama ni msomaji wa biblia utakuwa umekatana na hili neno sehemu nyingi..
Shokoa ni kiswahili cha zamani chenye maana ya “Vibarua”. Hususani wale waliotekwa na kulazimishwa kufanya kazi kwa nguvu.
Kwamfano katika biblia tunamwona Mfalme Sulemani, aliwachukua watu Shokoa..
2Nyakati 2: 7 “Basi kwa habari ya watu wote waliosalia wa Wahiti, na wa Waamori, na wa Waperizi, na wa Wahivi, na wa Wayebusi, wasiokuwa wa Israeli;
8 wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha SHOKOA HATA LEO”
Mistari mingine inayozungumzia juu ya shokoa ni 1Wafalme 5:13 , Yoshua 17:13, Waamuzi 1:28, Waamuzi 1:30 n.k
Na hata leo adui yetu shetani anawachukua watu Shokoa, kwa kuwateka na kuwatumikisha kwa nguvu. Anawatumikisha kwa dhambi, magonjwa, tabu na hofu.Wote aliowateka hawana raha, wala furaha, wala amani..Wamejawa na mashaka na kukata tamaa.. Yote hayo yanawapata kwasababu wamechukuliwa mateka (Shokoa) na adui shetani.
Lakini habari njema ni kwamba..Yupo mmoja ALIYETIWA MAFUTA NA MUNGU KUKOMESHA UTEKA. Huyo akikuweka huru umekuwa huru kweli kweli.. hofu yote itaondoka, hofu ya kifo, shida, tabu na magonjwa anaiondoa..na kisha anakupa raha nafsini mwako. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, KUWATANGAZİA MATEKA UHURU WAO, NA HAO WALİOFUNGWA HABARİ ZA KUFUNGULİWA KWAO.
2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao”
Ukimpokea maishani mwako, Uteka shetani aliokuteka, itakuwa ni zamu yako kumteka yeye…atakaa chini ya miguu yako, na ukimwambia ondoka ataondoka kwa hofu nyingi.
Kama hujampokea na utamani kufanya hivyo fuatiliza sala hii ya mwongozo wa toba kwa kufungua hapa >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/10/17/shokoa-ni-nini-katika-biblia/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.