by Admin | 27 February 2021 08:46 pm02
SWALI: tukisoma 2Mambo ya Nyakati 22:2.Inasema Hivi..
“Ahazia alikuwa na umri wa miaka AROBAINI NA MIWILI ALIPOANZA KUTAWALA; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri”.
NA tena Tukisoma 2Wafalme 8:26 inasema Hivi..
“;Ahazia alikuwa na umri wa miaka ISHIRINI NA MIWILI ALIPOANZA KUTAWALA; akatawala mwaka mmoja huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Athalia binti Omri mfalme wa Israeli”.
>>Hapa sijaelewa Kwenye Hizi Habari Kwa maana Kwenye 2Nyakati unasema Ahazia alianza kutawala akiwa na miaka 42 ila Kwenye 2Wafalme Inasema Ahazia alianza kutawala Akiwa na miaka 22..Naona Hii mistari Kama Inajipinga Yenyewe.
Umri hasaa wa Ahazia alipoanza kutawala ni upi?
JIBU: Vifungu hivyo vinaonekana kama vinajipinga, aidha kimojawapo kimekosewa au vyote, wengine wanasema ni hitilafu katika uchapishaji wa maandiko ya kale. Lakini kama ingekuwa ni hitilafu kwenye uchapishaji, ni wazi kuwa tangu zamani Wayahudi wangeshaliona hilo na kulirekebisha, kwasababu wale wapo makini sana katika uandishi wao, hususani katika mambo matukufu ya Mungu, lakini maandiko hayo yalikuwepo hivyo hivyo kwa maelfu ya miaka mbeleni. Na hawakuona hitilafu yoyote.
Lakini swali ni je, Ahazia alianza kutawala akiwa na umri wa miaka mingapi?
Ukweli ni kwamba alianza kutawala akiwa na miaka 22, kwasababu kama angekuwa ameanza kutawala akiwa na miaka 42, maandiko yangekuwa yamekosewa kwasababu utawala wa baba yake uliisha akiwa na umri wa miaka 40 (Soma 2Wafalme 8:17, 2Nyakati 21:20) . Hivyo, kama Ahazi angekuwa ameanza kutawala akiwa na umri wa miaka 42 basi angekuwa amemzidi baba yake kwa umri wa miaka 2 zaidi jambo ambalo haliwezekani kabisa.
Lakini ni kwanini, sehemu nyingine ionyeshe alianza kutawala akiwa na miaka 22, na sehemu nyingine miaka 42?
Zipo thathimini nyingi, lakini tukitazama historia fupi ya baba yake huyu Ahazia itatupa mwanga kidogo wa kuelekewa kwenye jibu letu. Baba yake huyu Ahazia aliitwa, Yehoramu. Yehoramu alikuwa ni mtawala mbaya sana mwenye uchu wa madaraka na ubinafsi, kwani hata Baba yake (Yehoshafati) alipokufa, licha ya kwamba aliwaachia mali nyingi yeye pamoja na ndugu zake, lakini pamoja na hayo alikwenda kuwaua wote, ili yeye avimiliki vyote.
Tendo hilo la kumwaga damu zisizokuwa na hatia za kuwaua ndugu zako, lilimuhuzunisha sana Mungu, ndipo Mungu akamlaani kwa kumpiga na ugonjwa huo usiokuwa na tiba wa kutokwa na utumbo.
Hivyo, hilo lilimfanya asiweze, kutawala vema katika hali ile ya kuugua..akawa kama mtu wa kukaa ndani tu aliyetengwa.
Sasa kumbuka na biblia haieleze kama alikufa kwanza ndipo mtoto wake, akachukua ufalme, hapana, inasema, alianza kutawala akiwa na miaka32, kisha akatawala miaka 8 tu. Lakini haisemi kwamba alikufa, hapana, kwahiyo pengine aliendelea kuishi, kwa kipindi kingine mbele akiwa kama mfalme asiyekuwa na kazi yoyote.
Hiyo ikapelekea wenyewe wa Yerusalemu kumfanya mwanawe kuwa mfalme, hivyo Ahazia akawa mfalme akiwa na umri wa miaka 22, lakini hakuwa mfalme kamili kabisa,kwasababu baba yake alikuwa bado hajafa. Ndipo alipokuja kufa huko mbeleni, Ahazia tayari alikuwa ameshafikisha umri wa miaka 42, ndipo wakamfanya kuwa mfalme kamili wa Yerusalemu. Akatawala miaka mmoja tu. Ambao ulianza kuhesabiwa katika umri wake wa 42
Hivyo biblia inaposema alianza kutawala akiwa na miaka 22 katika kitabu cha Wafalme, na miaka 42 katika kitabu cha Mambo ya Nyakati, biblia haijipingi, ni pengine tumekosa historia ya kutosha ya matukio yote ndani ya biblia ndio maana tunaona kama baadhi ya vifungu vimekosewa, lakini ukweli ni kwamba maandiko matakatifu hakuna mahali yalipokosewa..
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?
Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/02/27/mfalme-ahazia-alianza-kutawala-akiwa-na-umri-gani/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.