Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.

by Admin | 22 November 2021 08:46 am11

Mithali 25: 20 “Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi”.

Anaposema amwimbiaye nyimbo..anamaanisha nyimbo za furaha, au za shangwe kumwimbia mtu mwenye moyo mzito, kwa kudhania kuwa ndio zitatuliza uchungu wake, kumbe kinyume chake, ndio zinamwongezea masikitiko moyoni mwake.

Sulemani kwa hekima ya ki-Mungu aliliona hilo, kwamba, ni vema kuendana na hisia za mtu, kwamfano, kuna watu wapo katika uchungu mzito sana mioyoni mwao, pengine labda wa kufiwa  na mume/mke wake, au mzazi wake, au ndugu yake wa karibu sana, na wewe kwa mawazo yako ukaona ili kuwatuliza ni kwenda kuwachekesha, chekesha, au kuwaburudisha kwa nyimbo za furaha,..Ujue kuwa hapo hautatui tatizo. Ni lazima ujue hali ya mtu wakati huo, yupo katika uchungu wa namna gani.

Biblia inasema..

Warumi 12:15 “Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao”.

Lakini kama unaonyesha kufurahi pamoja na hao walioa, ukidhani ndio kiashiria cha kuwachangamsha..Ni rahisi kuwasha moto mwingine,

Kwasababu mtu Yule anaweza kudhani hujathamini hata kile anachokipitia, na matokeo yake atachukia badala ya kupona,..Ni ndio hapo anasema sawa na kumvua mtu nguo zake wakati wa baridi kali, ni nini kinatokea? Ni mateso zaidi kama sio kifo.

Kwahiyo tuwe na hekima ya kujua ni dawa ipi tunaitumia kumponya mtu aliyevunjika moyo. Ikiwa kweli anahitaji, furaja za nyimbo tutumie hizo, lakini kama yupo katika uchungu mwingi sana wa moyo, tuendane na hisia zake, hiyo ndio dawa pekee ya kuwaponya watu kama hao.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

SIFONGO NA SIKI NI NINI?

Nini maana ya Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu?

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

 Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”

Zaburi maana yake nini, katika Biblia?

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/11/22/amwimbiaye-nyimbo-mtu-mwenye-moyo-mzito/