IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!

by Admin | 16 January 2020 08:46 pm01

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Biblia..

Jambo mojawapo ambalo shetani anapenda kulitumia ili kuikatisha kazi ya Mungu ni kutumia vitisho?..Kwamfano utaona katika agano la kale wakati fulani ambapo Mungu aliwarudisha tena wana wa Israeli katika nchi yao baada ya kukaa utumwani Babeli kwa muda wa miaka 70 aliwaagiza watakaporudi wamjengee nyumba….Na kweli waliporudi walianza harakati za kuijenga nyumba ya Bwana huo Yerusalemu.Lakini kilichotokea ni kwamba..kazi ile haikudumu kwa muda mrefu..kwani maadui zao baada ya kuona wanaijenga nyumba ile waliwainulia visa…ikiwemo kwenda kupeleka taarifa kwa Mfalme kwamba watu baadhi fulani wanaijenga nyumba ambayo ilibomolewa kwa makusudi fulani…Hujuma zile zilipomfikia Mfalme akatoa amri kazi ile isimamishwe mara moja…Na wale watu wakamwogopa mfalme wakaacha kuifanya ile kazi..

Ezra 4:11 “Hii ndiyo nakili ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta; watumishi wako,watu walio ng`ambo ya mto wakadhalika.

12 Ijulikane kwa mfalme ya kuwa Wayahudi, waliokwea kutoka kwako, wamefika kwetu Yerusalemu; nao wanaujenga ule mji mwasi, mbaya; wamemaliza kuta zake, na kuitengeneza misingi yake.

13 Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.

14 Na sisi, kwa kuwa tunakula chumvi ya nyumba ya mfalme, wala si wajibu wetu kumwona mfalme akivunjiwa heshima, basi tumetuma watu na kumwarifu mfalme.

15 Ili habari zitafutwe katika kitabu cha tarehe za baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu cha tarehe ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na maliwali, na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu mji huo ukaangamizwa.

16 Twamwarifu mfalme ya kuwa mji huo ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hutakuwa na sehemu ya nchi ng’ambo ya Mto.

17 Ndipo mfalme akapeleka majibu;Kwa Rehumu,Bwana shauri, na Shimshai,mwandishi na wenzao wengine waliokaa katika Samaria,na penginepo ng`ambo ya mto, Salamu; wakadharika.

18 Ule waraka mlionipelekea umesomwa mbele yangu, nami nikaelewa na maana yake.

19 Nikatoa amri, na watu wametafuta habari; ikaonekana ya kuwa mji huu zamani umefanya fitina juu ya wafalme, na ya kuwa uasi na fitina zimefanyika ndani yake.

20 Tena walikuwako wafalme wakuu juu ya Yerusalemu, waliotawala nchi yote iliyo ng’ambo ya Mto; wakapewa kodi, na ada, na ushuru.

21 Sasa toeni amri kuwakomesha watu hawa kazi yao, mji huu usijengwe, hata mimi nitakapotoa amri. 22 Tena jihadharini, msilegee katika jambo hili; kwa nini madhara yazidi, na wafalme wapate hasara?

23 Hata nakala ya waraka huo wa mfalme Artashasta uliposomwa mbele ya Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.

24 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu ikakoma; nayo ikakoma hata mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi”.

Kama tunavyoona tendo hilo likawafanya wayahudi waiogope amri ya mfalme Zaidi ya maagizo ya Mungu ambayo waliambiwa waijenge nyumba ile bila woga!..Wakaendelea kukaa katika hali hiyo kwa muda mrefu mpaka Mungu alipozifunga mbingu mvua ziwe chache na chakula cha shida, Mpaka Mungu alipowatuma tena manabii wake Zekaria na Hagai kuwaambia watu watoke wakaijenge nyumba ya Mungu pasipo kuogopa chochote na Bwana atakuwa nao. Na walipowatii manabii wale walitoka na kwenda kukusanya vifaa vyote na vitu vyote vya ujenzi tayari kuanza kazi bila kujali tamko la mfalme..wakati wanaanza wale maadui zao tena wakapata taarifa na kumpelekea mfalme…

Lakini Mungu aliugeuza moyo wa mfalme kwa namna isiyoelezeka badala ya kuwapinga wayahudi kinyume chake alikubaliana nao..na zaidi ya yote akawafadhili kwa mali katika ujenzi wao..hivyo nyumba ya Mungu ikajengwa na kusitawi pasipo shida yoyote..Na Mungu akawabariki Israeli.

Ezra 5:1 “Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli.

2 Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.

3 Wakati ule ule Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu?

4 Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani na nani?

5 Lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie, hata habari ile imfikilie Dario, ndipo jawabu litakapopatikana kwa waraka.

6 Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Dario; na Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng’ambo ya Mto,

7 walimpelekea waraka nao; na maneno haya yakaandikwa ndani yake; Kwa Dario, mfalme; Salamu sana.

8 Na ajue mfalme ya kuwa sisi tuliingia nchi ya Yuda, tukafika kunako nyumba ya Mungu mkuu, iliyojengwa kwa mawe makubwa, na miti imetiwa katika kuta zake, na kazi hii inaendelea kwa bidii, na kusitawi katika mikono yao.

9 Ndipo tukawauliza wale wazee, tukawaambia hivi, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu?

10 Tukawauliza pia majina yao, ili kukuarifu wewe, tupate kuandika majina ya watu waliokuwa wakubwa wao.

11 Wakatujibu hivi, wakasema, Sisi tu watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunaijenga nyumba iliyojengwa zamani sana, yapata miaka mingi, ambayo mfalme mkuu wa Israeli aliijenga na kuimaliza.

12 Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli.

13 Lakini katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Babeli, Koreshi, mfalme, alitoa amri ijengwe tena nyumba ya Mungu.

14 Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, alivyovitoa Nebukadreza katika hekalu lililokuwako Yerusalemu, na kuviingiza katika hekalu la Babeli, vyombo hivyo mfalme Koreshi alivitoa katika hekalu la Babeli, akakabidhiwa mtu, jina lake Sheshbaza, ambaye alikuwa amemfanya liwali;

15 naye akamwambia, Chukua vyombo hivi, uende, ukavitie katika hekalu lililoko Yerusalemu, na nyumba ya Mungu na ijengwe mahali pake.

16 Ndipo ye yule Sheshbaza alipokuja, akaupiga msingi wa nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na tangu wakati ule hata leo imekuwa ikijengwa, wala bado haijamalizika.

17 Basi, sasa, mfalme akiona vema, watu na watafute katika nyumba ya hazina ya mfalme, iliyoko huko Babeli, kama ni kweli ya kuwa mfalme Koreshi alitoa amri kuijenga nyumba hiyo ya Mungu katika Yerusalemu, na mfalme akatuletee habari ya mapenzi yake katika jambo hili”.

EZRA 6:1 Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli.

2 Na chuo kimoja kilipatikana huko Akmetha, katika nyumba ya mfalme iliyo katika wilaya ya Umedi, na ndani yake maneno haya yameandikwa ili yakumbukwe.

3 Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini;

4 ziwepo safu tatu za mawe makubwa, na safu moja ya miti mipya; gharama zake zitolewe katika nyumba ya mfalme.

5 Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, ambavyo mfalme Nebukadreza alivitoa katika nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu, akavileta mpaka Babeli, na virudishwe, vikaingizwe tena katika hekalu lililoko Yerusalemu, kila kimoja mahali pake, na wewe uvitie katika nyumba ya Mungu.

6 Basi sasa ninyi, Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng’ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale;

7 iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake.

8 Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng’ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe.

9 Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng’ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa;

10 wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima.

11 Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili.

12 Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi.

13 Ndipo Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao.

14 Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi.

15 Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario”

Unaona, Lakini endapo wangekaa na kuendelea kusubiri..huku wanaiogopa amri ya mfalme..wangeendelea kukaa katika hali ile ile na hakuna chochote kingetokea…

Hivyo inatufundisha kuwa…tusiogope Kuifanya kazi ya Mungu maadamu ni yeye ndiye aliyetuagiza…Bwana Yesu alisema…

Mathayo 28:19 “ Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI”.

Yupo pamoja nasi…haijalishi sheria ya nchi imesema tusihubiri…Hilo haliwezi kutuzuia sisi kuhubiri, haijalishi watu wanasema tusihubiri hiyo haipaswi kutufanya sisi tusihubiri..Haijalishi tayari kuna mswada ulipitishwa wa injili isihubiriwe…Injili itahubiriwa tu..Katika kuhubiri huko Bwana amesema atakuwa pamoja na sisi..Kama alivyokuwa na wayahudi hao hhapo juu.

Tujifunze tena katika habari hii ya mwisho..katika tutapata moyo zaidi katika kwenda kuhubiri habari njema…

Tusome…

Matendo 5:17 “Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,

18 wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;

19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,

20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.

21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.

22 Hata watumishi walipofika hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari,

23 wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua hatukukuta mtu ndani.

24 Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo.

25 Mtu mmoja akaja akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu.

26 Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga kwa mawe.

27 Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,

28 akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.

29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti.

31 Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio”.

Katika habari hiyo unaweza kuuliza… “kwanini malaika wamevunja sheria ya nchi?”…Kwasababu wamewatoa watu gerezani kinyume na utaratibu na bado wanawarudisha wahalifu wakafanye yale yale waliyozuiliwa kuyafanya tena kule kule hekaluni wanapopingwa.

Hebu jiulize umekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa fulani…na usiku malaika anakuja kukutoa mahabusu pasipo ripoti yoyote na kukuambia ukaendelee kufanya kile kile kitu ambacho umezuiliwa kukifanya…Unaona hilo linaingia akilini?..kwasababu biblia inasema pia “tutii mamlaka iliyokuu”..Sasa kwanini hapa mamlaka hiyo inavunjwa?.

Jibu ni kwasababu ipo mamlaka nyingine iliyo kuu Zaidi ya hiyo ambayo ilishasema “Tukahubiri Injili kwa kila kiumbe, na yeye atakuwa na sisi hata ukamilifu wa Dahari”. Hakuna mamlaka nyingine duniani, wala kuzimu ambayo inaweza kuzidi hiyo Amri. Hakuna kikundi chochote, wala chama cha siasa, wala dini,wala wenye mamlaka, wala serikali yoyote ambayo ipo juu ya hiyo AMRI.. Na wala hakuna chochote kinachoweza kuizuia isitekelezeke.. Injili itahubiriwa tu mamlaka ya nchi ipende au isipende..Amri iwe imetolewa au haijatolewa…iwe imehalalishwa au haijahalalishwa…Yesu Kristo yupo upande wa wanaoihubiri injili haijalishi ni vikwazo vingapi vinaonekana mbele..haijalishi kuna hatari kiasi gani endapo itahubiriwa…lakini Injili(yaani Neno la Mungu)…Litahubiriwa tu..Bwana Yesu Kristo atahakikisha inafika kwa kila kiumbe…na hiyo ni AMRI sio OMBI. Kwasababu mamlaka yote ya mbinguni na duniani kapewa yeye..na hakuna aliye juu yake.

Hivyo simama hubiri injili leo..usiangalie mazingira yanayokuzunguka..usiangalie hatari zinazokuzunguka..yeye amesema “atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa dahari”…

Warumi 8:31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?”.

Ubarikiwe sana.

Kama hujaokoka..simama leo uokoke…Tubu kwa dhati na kusudia kuacha yote uliyokuwa unayafanya yaliyo kinyume na Neno la Mungu. Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312

Mada Nyinginezo:

KUTOKUIHUBIRI INJILI,KUNA MADHARA GANI?

 

 

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NI MPANGO WA MPINGA-KRISTO.

AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

 

MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/01/16/ifanye-kazi-ya-mungu-pasipo-hofu/